DAR ES SALAA, Tanzania
BENDI ya Muziki wa
Dansi hapa nchini, Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ juzi usiku ilitambulisha
nyimbo zake mbili Mgeni na Hafidhi katika ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam.
Wimbo wa Mgeni
umetungwa na Khadija Kimobitel huku Hafidhi unozungumzia jina la kijana mmoja
ukitungwa chini ya mtunzi Athanas Michael.
Nyimbo hizo zilionekana
kuwavutia wadau mbalimbali wa muziki huo walioudhulia shoo hiyo, na kujikuta
wakiwatuza wanenguaji wa kiume ambao walionyesha shoo ya kuvutia hadi mashabiki
kupigwa na butwaa na kushindwa kucheza.
Akizungumzia nyimbo
hizo, Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema, huu ni mwanzo kwani bendi
yake imejipanga ipasavyo kuachia ngoma nyingi kabla ya mwaka hu kumalizika.
“Hizi nyimbo mbili
na watunzi tofauti, na lengo kubwa na kuwapa vitu vya tofauti mashabiki wangu,
wasiboleke na nawahaidi kuendelea kuwapa burudani mulua zaidi,”alisema Choki.
Nae Shabiki mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Husna Abdallah alisema, mwanzoni alikuwa
anakwenda bendi mbalimbali ambazo hakutaka kuzitaja na kudai kuwa amevutiwa na
Extra bongo jinsi ambavyo wanaimba mpaka wanenguaji walio nao.
No comments:
Post a Comment