Na Francis Godwin,Iringa
Mkazi wa Mwangata B katika Manispaa ya Iringa Vumilia Sanga (35) amepoteza maisha yake baada ya kuanguka kutoka juu ya mti wakati akichuma matunda aina ya mapera nje ya nyumba yake .
Tukio hilo limetokea jioni ya juzi majira ya saa 10 baada ya mwanamke huyo ambae anasadikika kuwa alikuwa akishumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana wakazi wa eneo hilo wakiwemo ndugu wamedai kuwa kabla ya kifo chake marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa na inawezekana tatizo hilo lilimkuta akiwa juu ya mti huo na hivyo kuanguka na kuchomwa na mti mgongoni na kutokea tumboni .
Alisema mkazi wa eneo hilo alijitambulisha kwa jina la Adam Kalinga kuwa kutokana na mwanamke huyo kuanguka juu ya mti majirani walijaribu kutaka kumwokoa ila baada ya kusogea walikuta tayari utumbo na maini yakiwa nje na kabla hata ya kumgusa alikata roho .
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa mwangata B Julius Lwimbo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa hadi majira ya saa 11.45 jioni polisi walikuwa bado hawajafika eneo la tukio ili kuutoa mwili huo .
Pia mwenyekiti huyo amekiri kuwa ni kweli mkazi huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa na kuwa yawezekana kuanguka kwake kumetokana na tatizo la ugonjwa huo na kuwa baada ya kuanguka toka juu ya mti aliangukia katika jiti ambalo lilikuwa limechongoka na ndilo limemtoa uhai wake .
No comments:
Post a Comment