March 31, 2013

NSSF QUEENS YAICHAPA ZSSF QUEES 35-29 KATIKA BONANZA LA PASAKA

 Kikosi cha ZSSF Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na NSSF Queens katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana mjini Zanzibar.  (Picha na  Habari Mseto Blog)
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifungua mashindano ya tamasha la Pasaka kwa timu za netiboli yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar na kuzikutanisha timu za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF)
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifuatilia kwa makini mchezo wa netiboli wa tamasha la Pasaka kati ya ZSSF na NSSF uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi Mwendeshaji ZSSF, Abdulwakili Haji Hafidh na Kulia ni Meneja Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli na wa pili  kulia ni Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori .
 Barke Mohamed wa ZSSF (katika) akichuana na mchezaji wa NSSF Queens
 Mchezaji wa NSSF, Matalena Mhagama akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa ZSSF Queens, Barke Mohamed.
Mashabiki wa timu ya NSSF Queens wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga ZSSF Queens 35-29 katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kweye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Asha Seif Idd akimkabidhi ngao ya ubingwa wa michuano ya Tamasha la Pasaka, nahodha wa timu ya NSSF Queens, Pili Rashid Mogella baada ya kuifunga ZSSF 35-29.
Naodha wa timu ya NSSF Queens, Pili Rashid Mogella akimkabidhi ngao ya ubingwa wa tamasha la Pasaka Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume baada ya kuifunga ZSSF magoli 35-29 katika mchezo uliofanyika katika viwanja vya Gymkana mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Meneja Uwekezaji na Mipango NSSF, Abdallah Mseli.
Kikosi cha timu ya NSSF Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na ZSSF Queens. NSSF Queens ilishinda 35-29.

No comments:

Post a Comment

Pages