Ratiba ya mechi za robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa leo mchana.
MONACO, Ufaransa
Aidha, ratiba ya michuano ya Europa League pia
ilipangwa jana pia, ambapo Chelsea itatoana jasho na Rubin Kazan, Tottenham
Hotspur itapimana ubabu na FC Basel Uswisi, huku Fenerbache ikicheza na Lazio nayo
Benfica ikikipiga nma Newcastle.
HATIMAYE kitendawili cha mechi
za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kimeteguliwa leo mchana, baada ya
kukamilika kwa tukio la upangaji ratiba, ambayo licha ya kuingiza timu tatu,
klabu za Hispania zimefanikiwa kukwepana.
Katika ratiba hiyo, Malaga ya Hispania itaanzia nyumbani kuumana na Borussia
Dortmund, kama itakavyokuwa kwa Real Madrid,
iliyopangwa kukipiga na Galatasaray iliyo na nyota wa zamani wa Galacticos,
Wesley Sneijder.
PSG ya Ufaransa itakuwa na
kibarua kipevu kilichowashinda AC Milan, wakati watakapowaalika FC Barcelona ya
Hispania, huku, Bayern Munich ya Ujerumani ikitarajia kutoana ngeu na ‘Kibibi
Kizee’ Juventus Turin.
Mechi za robo faibali za
michuano hii zinatarajia kupigwa Aprili 2 na 3, ambapo mechi kati ya Malaga dhidi ya Dortmund na
ile ya Madrid
na Galatasaray zitapigwa Jumanne Aprili 2, huku PSG dhidi ya Barca na ile ya
Bayern na Juve itapigwa Jumatano Aprili 3.
Marudiano ya mechi hizo
yatakuwa Apili 9 na 10, kusaka miamba minne itakayocheza nusu fainali ya
michuano hiyo, itakayopigwa mwishoni wa mwezi ujao na kurudiana Mei mwanzoni,
kusaka tiketi ya fainali Mei 25 kwenye Uwanja wa Wembley.
Aidha, ratiba ya michuano ya
Europa League pia ilipangwa leo katika hafla hiyo, ambapo Chelsea
ya England itatoana jasho na
Rubin Kazan ya Russia, huku
Tottenham Hotspur ya England
ikipimana ubabu na FC Basel Uswisi.
Fenerbache ya Uturuki itakuwa
na kibarua dhidi ya SS Lazio ya Italia, huku Benfica ya Ureno ikikamuana na Newcastle ya England. Mechi za kwanza robo
fainali hii zitapigwa Alhamisi ya Aprili 4 na marudiano yatakuwa Aprili 11.
Uefa.com
No comments:
Post a Comment