March 20, 2013

Samsung yazindua Galaxy Camera


 Mpiga Picha Mkuu wa Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Sayari na Tanzania daima, Joseph Senga (kushoto) akiangalia aina mpya ya Samsung Galaxy Camera wakati wa uzinduzi wa camera hiyo jijini Dar es Salaam. 

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Samsung Tanzania, juzi usiku imezindua rasmi bidhaa mpya ya Samsung Galaxy Camera, ambapo kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Vodacom wameweka kifurushi cha 1GB kwa muda wa miezi mitatu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam juzi, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar, alisema kuwa, Samsung Galaxy Camera ni zaidi ya simu yenye kamera kiutendaji na ubora wa huduma zake.

Aliongeza kuwa, Samsung Galaxy Camera, ina CMO sensor, ambayo inawezesha kamera hiyo kuchukua picha zenye ubora wa hali ya juu.

Katika uzinduzi huo wa Galaxy Camera, ambayo ni ya kisasa zaidi, Minhai Patel aliibuka na zawadi ya aina hiyo mpya ya kamera katika droo ndogo iliyoshirikisha waalikwa waliohudhuria uzinduzi.

Kwa upande wake, Meneja Usambazaji na Mauzo wa Samsung Mobile, Sylvester Manyara, alisema kuwa, Galaxy Camera ina tofauti na kamera nyingine, kwa sababu yenyewe inatumia mtandao wa 3G, unaoiwezesha kupata huduma ya Internet ya kasi.

Aliongeza kuwa, Galaxy Camera ina uwezo wa kutuma picha hadi katika mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Whatsapp na Instagram na kwamba kamera hizo zinatoa picha za ubora zaidi hata zilizopigwa kutoka umbali mrefu.

No comments:

Post a Comment

Pages