March 12, 2013

Wenye vituo vya TV wasiburuzwe na digitali za watu

Na Bryceson Mathias

KUTOKANA na wananchi wengi wasiokuwa na uwezo wa kununua ving’amuzi; Wenye vituo vya TV wasikubali kuburuzwe na digitali za watu, wakati mapato ya matangazo yao yanapungua na gharama za uendeshaji kuwa kubwa,  hivyo kutishia vituo vyao kujifunga vyenyewe, kwa kukosa watazamaji.

Uchache wa watazama TV, unafuatia wengi wa wateka kurejea kuburudika na Video na mikanda ya nyimbo za Dini na kusikiliza Habari kwenye Radio, ambapo wanaona ni heri kuwa na mikanda ya CD na DVC za dini, kuliko kununua King’amuzi kinachomgharimu fedha nyingi wakati hawajiwezi.

Toka awali tulisema, watendaji walioiga mtindo huo ambao kimsingi ni mzuri, wamekurupukia kufunga mitambo ya Analogia mapema bila kuzingatia wateja wao kuwa ni walalahoi na sio walalahai, kwa maana kwamba, hawawezi kumudu king’amuzi cha Laki 5/-, watoto wao walale na njaa.

Mmoja wa watazamaji TV aliyedai labda wadau wa mabadiliko hayo walikusudia kuua biashara hizo alisema, “Huwezi kung’ang’ana wanachi wako wanunue King’amuzi cha Ma-Laki ya fedha ukijua  watoto wanashindwa kwenda shule, wanakula mulo moja au wanashindia na kulalia wadudu wa Kumbikumbi”.

Hakuna mtu mbaya kama mtu anayetupa Chakula wakati Jirani yake analala na Njaa. Wadau wa Digitali wanaona ni heri watanzania walalahoi, waliojinusuru wakanunua TV vijijini na kuweka Solar ilimradi waweze kuhabarishwa, ghafla wahamishwe na kukomolewa kwa kukatiwa matangazo.

Kama karibu watanzania Hoi karibu 70% vijijini walikuwa hawajaweza kupata mawasiliano ya TV kwa njia ya Analogia, inakuwaje wanakatiliwa na kuwalazimisha wakimbia kabla hata ya kusimama Dedee wakati hawana kipato?.

Kama majirani zetu na nchi zingine za kiafrika na nchi zinazoendelea hawajafikia kuzima mitambo yao kutokana na kuwajali watu  wao ili kwanza watembee dede, mbona nchi yetu na watendaji wake wana kiherehere, cha nini? Au kuna mkono wa mtu anafanya biashara na kurudisha fedha zake?.

Je, wadau wanaofanya hivyo, wana tofauti ya namna gani na wale wanaofanya watoto wetu waende Kidato cha kwanza wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu?

Ni wazi hao hawana tofauti na wanaowapa Elimu watoto wetu bila Mitaala Maalum, halafu wanawatungia mtihani migumu, kama wa ving’amuzi wakiwani maskini wa kutupwa.

Hakuna Mdau au Polisi anayeweza kumlazimisha mtu kuoa au kuolewa wakati muda wake haujafika au hajajiandaa kukabili changamoto za Uenzi wa Ndoa ikiwa ni pamoja na kuwa na kipato. Samani, nyumba na Ardhi kulima au biashara ya kumuongezea kipato ili ajikimu.

Ni rai yangu kama wenye Vituo vya TV wanaweza kuwa na Upendo wa Agape kiasi cha kuwahabarisha na kuwaburisha watanzania bila kupata hasara, ni vema wakafanya hivyo ili wamebakikiwa kwa kuwasaidia na kuwajali watu hata katika ulalahoi wao.

Kama nilivyosema awali, watazamaji TV walio wengi wamerejea kwenye Radio Cassette na Mikanda ya Video ya awali, kusudi kubwa likiwa ni wasikilize nyimbo za Dini na nyinginezo.  

Kwa namna hiyo, nimebaini kwamba Biashara ya Kanda za Cassette na Video, hivi sasa imeanza kushamiri sana na marejesho yake agharabu ni mazuri sana kwa wachunguzi, ingawa naamini wenye vituo vya TV wanapata  hasara uendeshaji wake.

Ieleweke; Mwenye Chongo mbele ya Kipofu, ni Bosi na ni Mfalme. Tukumbuke kurupuko la vithibiti mwendo

Mwandishi wa Makala hii anapatikana kwa 
0754933308

No comments:

Post a Comment

Pages