April 03, 2013

POLISI WATULIZA VURUGU ZA CCM NA CHADEMA, NI ZA UCHAGUZI WA MABARAZA YA KATA

Ispekta Generali wa Polisi (IGP), Said Mwema.

Na Bryceson Mathias, Mvomero
JESHI la Polisi wilayami Mvomero, limefanikiwa kutuliza vurugu za uchaguzi wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya (Mamlaka za Serikali za Mitaa) na uendeshaji wake uliotangazwa na tume ya mabadiliko ya katiba.

Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike jana  Kichamgani Turiani, ulkwama kufanyika, baada ya kuibuka vurugu wananchi wakimkataa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho Bw. Damson Minja asiwe Mwenyekiti wa kikao kwa sababu ameshindwa kusoma mapato na matumizi tangu achaguliwe.

Diwani wa Kata ya Mhonda Bw. Salum Mzugi na viongozi mbalimbali wa CCM walishindwa kutuliza na kurejesha Amani kwa sababu badala ya kutatua Vurugu hizo kwa kufuata Mwongozo, taratibu na Sheria za Uchaguzi huo, walitanguliza Itikadi jambo lililosababisha Polisi kuingilia Kati wakiwa tayari na Mabomu ya Machozi.

“Vurugu ilifikiwa pale Viongozi wa CCM walipolazimisha Wananchi waongozwe na Mwenyekiti Minja wasiyemtaka ambapo walishatangaza kumng’oa kwa kushindwa kusoma mapato na matumizi tangu achaguliwe 2010. Hivyo Chadema kuona CCM inataka kuwaburuza”.alisema Diwani wa Viti Maalum Bi. Juliana Petro (CHADEMA).

Sinema iliyokuwepo kwenye Kiti cha Mwenyekiti ilikuwa, Mwenyekiti Bw. Minja akitaka kukaa kwenye kiti, Kiti hicho kilikuwa kimavutwa na Wananchi wanaopinga, Jambo lilizua ubishani wa kisiasa baina CCM na CHADEMA, hadi kusababisha viongozi hao wa Mabaraza kutochaguliwa.

Aidha Jeshi la Polisi Kituo cha Turiani kupitia kwa Kamanda Rajab Shemndolwa liliagiza, viongozi husika watafute mwongozo wa Taratibu na Sheria zinazotakiwa kufuatwa katika kutatua mgogoro huo toka kwenye vyombo husika, ila hawataki vurugu, na zikitokea hawatasita kuchukua hatua za maamuzi magumu.

Mgogoro wa wananchi wa Kichangani Turiani kumkataa Mwenyekiti wao Bw. Minja, umedumu kwa miaka mitatu sasa bila kutatuliwa na viongozi husika katika kata na wilaya ya mvomero, tatizo likiwa ni Serikali ya mwenyekiti huyo kutosoma Mapato na Matumizi jambo ambalo lisipotatuliwa, linaweza kuleta maafa baadaye.

No comments:

Post a Comment

Pages