April 03, 2013

'KIDEALA' YA MEZ B YAANZA KUTESA


Na Elizabeth John
MKALI  wa muziki wa kizazi kipya nchini, Moses Bushagama ‘Mez B’ ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Kidela’ ambacho kimeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Mez B alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Kama vipi’ alichoimba na mwanadada Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambacho kilifanya vizuri zaidi mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vilitamba kipindi hicho.

Akizungumzia kazi hiyo mkali huyo alisema aliifanya na marehemu Sharo Milionea lakini kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wao walishindwa kuitoa kwa wakati na kulazimika kuitoa kipindi hiki.

“Kazi hii niliifanya na mkali wa muziki huo marehemu Sharo lakini kuna vitu viliingiliana tukashindwa kuachia kwa wakati, lakini baada ya kufariki kwa msanii huyo nilishindwa kuitoa nikaona nitafute mtu mwingine badala yake,” alisema Mez B.

Mez B alisema kwasasa yupo katika maandalizi ya kufanya video ya wimbo huo ambayo anaifanyia katika studio ya Smart Music chini ya mtayarishaji wake Mbezi, iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam.

Pia aliwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hiyo ambayo ipo katika hatua za mwisho za uandaaji ikiwa ni pamoja na kazi nyingine ambazo zinafuata.

No comments:

Post a Comment

Pages