April 02, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS WA KENYA WILLIAM RUTO


 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka. (PICHA NA IKULU)


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS WA KENYA  WILLIAM RUTO MBUGANI SERENGETI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe. William Kipchirchir Samoei arap Ruto  ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Kitalii ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti  mkoani  Mara, Rais Kikwete  amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.

Mhe Rais pia alimuelezea Mhe Rutto  juu y furaha yake pamoja na kuridhishwa  na jinsi  uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.

Alielelezea  matumaini yake ya kuwa  urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya  utadumishwa  pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani  Mara wiki  iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka  leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.

 Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Aprili,  2013

No comments:

Post a Comment

Pages