April 02, 2013

Tuhuma zinazomkabili Meya Amani Bukoba, Ndizo zimuondoe!


Na Bryceson Mathias 

'Wapiganapo Fahari Wawili Nyasi Huumia'
 
WAKATI Mgogoro kati ya Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Dk. Anatory Amani (CCM), na baadhi ya madiwani wa chama hicho, umekigawa pia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bukoba Mjini; Tuhuma zinazomkabli ndizo zimuondoe kwa faida ya wananchi.

Ingawa CHADEMA kupitia viongozi wake wa wilaya ya Bukoba Mjini wakiwemo madiwani wake wanne, ndio walioiasisi hoja ya kupinga miradi ya kifisadi iliyoingiwa na Amani pasipo kufuata utaratibu wa kisheria; Sera za Chadema kwa wananchi wake; Ufisadi si Rafiki yake!.

Kutokana na uhamasishaji wa mikutano ya hadhara, uliofsnyes ns viongozi wa Chadema kuwaelimisha wananchi hasara itakayotokana na utekelezaji wa miradi iliyoingiwa kinyume na Amani, licha ya upinzani toka kwa Meya na madiwani wa CCM, uwepo wa Ufisadi uwe Kigezo.

Hata kama sasa Serikali imeunda tume ya kuchunguza tuhuma za madiwani ambao wanadai Meya Amani anatekeleza miradi mbalimbali katika mazingira ya kificho, viongozi wa Chadema wasikubali Sera za Chama kuuchukia Ufisadi kikaonekana kinaukumbatia ni kukidharirisha 

Pengine ni Nia yangu kuona kwamba, Viongozi wa Chadema Bukoba wasione kama kuridhia Meya ang’oke ni kumpalilia Unga wa Mjengoni Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki, la Hasha! Bali ni kuenzi msimamo wa Chadema na Sera za kupinga Ufisadi nchini.

Miradi iliyotajwa kwenda ndivyo sivyo ambayo ya upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhama ya Uwekezaji (UTT) kuwa haukufuata taratibu na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.

Tuhuma za mradi wa ujenzi wa soko ambao Meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.

Tuhumiwa ya kukopa sh milioni 200 kutoka Benki ya Uwekezaji (TIB) bila kibali cha Baraza la Madiwani, na kwamba pia alitoa taarifa kwenye kikao cha baraza hilo kuwa TIB iliwapa ruzuku ya sh milioni 90, lakini hakueleza misingi yake! Vyote hivyo Chadema ielewe ni Haki ya Taifa.

Ilielezwa pia uko mradi wa kuosha magari ambao unadaiwa kutumia kiasi cha sh milioni 297 zinazotiliwa shaka, na kwamba pia ameshindwa kutoa mchanganuo wa mapato na matumizi ya miradi ya kiasi cha sh milioni 134 ya ujenzi wa kituo cha mabasi.

Viongozi wa Chadema Bukoba wasipumbazwe na kukosana kwa Meya Amani na Mbunge Kagasheki kiasi cha kuwafanya waharibu Heshima ya Chadema dhidi ya Ufisadi, bali nawataka wakumbuke katika Biblia wakati wa kumsulubisha Farao Pilato na Farao walipatana.

Lakini pia nilipendaniwaase Chadema Bukoba kwamba Maziwa Hayaungwi Pilipili, hivyo wanachojaribu kukifanya sasa hadi kuupasua msimamo wa kuwatete wananchi kwa vigezo visivyo na mashiko, ni kuunga Pilipili Maziwa (Rasilimali) ya wana Bukoba ili ichakachuliwe.

Ni rai yangu akumbuke Tabu na Mateso ya Wana Bukoba, ambayo nakumbuka katika Vita vya Kagera dhidi ya Fashisti Idd Amini Dada ambayo nilishiriki kikamilifu toka Kyaka hadi Kitgum-Uganda, nilishuhudia Uchumi wao ukiharibiwa, hivyo fursa ya kuurejesha iheshimiwe.

Ni katazo langu pia kwa viongozi wa Chadema Bukoba, wasithubutu kufurahia Mikate ya Blue Band na Mapande ya Nyama waliyokula wana wa Israel kwa Farao kiasi cha kusahau mateso na adhabu za kugonga Mawe walizozipata, hadi Musa alipowaondoa utumwani.

Ni furaha yangu wana Bukoba wanavushwa Ng’ambo ya Bahari ya Shamu kuliko na Maziwa na Asali, ili wafurahie ukombozi wao, kuliko kubaki katika mateso ambayo wagombanao wanaweza kupatanishwa na Chama chao,  Ninyi mkaaibika.

Ishara za ukweli ninaousema, kumbukeni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philipo Mangula, alifika Bukoba Februari mwaka huu, na kukutana na uongozi wa CCM Wilaya wakiwemo madiwani na kuwaagiza waondoe tuhuma zao dhidi ya meya akidai walikiuka utaratibu.

Ingawa hatua hiyo ilikuza mgogoro na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye, kulazimika kuingilia kati kwa kuiomba Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuunda tume ya kuchunguza tuhuma hizo; kwa vigezo hivyo hivyo Chadema muelewe wanaweza wakapatana mkapaki na aibu.

Muondoeni Meya kwa Tuhuma zake, si kwa kumuangalia Kagasheki kwa Ubunge na Sifa mnayodhani anaipalilia, Bali achane Ngano ikue na Magugu 2015 mtazifunga  Matita AMatita na kuyachoma Moto.
0715-933308

No comments:

Post a Comment

Pages