April 03, 2013

Ukitaka Kuikosoa Serikali ya CCM Jiunge CHADEMA


Na Bryceson Mathias, Mvomero.
 
ALIYEKUWA Katibu wa Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilayani Mvomero Dismas Ngeresha amesema, mwana mapinduzi yeyote anayetaka kuikosoa serikali ya chama cha Mapinduzi CCM, ajiunge Chadema.
 
Dismas alisema hayo jana akiwa Manyinga Mvomero alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na kuwepo upepo mbaya  kwake wa kisiasa, ambapo yeye anapingwa na Viongozi wa CCM kijijini hapo asiwe Katibu wa Kamati ya kuchunguza Uvamizi wa Mipaka ya Shule ya Msingi Manyinga ‘A’ na ‘B’ .
 
Uvamizi huo unadaiwa ulifanywa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho (CCM) akituhumiwa kupora na kujenga nyumba ndani ya eneo la eneo la shule hiyo, umechukua Sura mpya ambapo Mwenyekliti Regina Mathias na Mtendaji Hssan Dega wanapinga Ngeresha (CHADEMA) kuwa kwenye Kamati.
 
“Mwandishi; Nasema hivi, ukitaka kuikosoa Serikali ya CCM jiunge Chadema,; huu ni wito kwangu kwa wananchi na viongozi wote nchini kwamba huwezi kuikosoa Serikali na CCM ukiwa Gamba, lazima uvue Gamba uvae Gwanda. Hawa CCM, wanataka kisicho sahihi useme ni sahihi” alisema Ngeresha.
 
Mwenyekiti Mathias, Mtendaji Duge na Mwalimu Mkuu Salum Hembe, kwa pamoja wanakiri kuwepo kwa Tuhuma za wananchi kulalamikia Uvamizi wa maeneo ya Shule za Msingi za Manyinga A na B, na kujengwa nyumba ambapo Makundi Mawili ya SadiQ Murad na Amosi Maklla (MB), yalihasimiana.
 
Aidha Majina ya Kamati iliyoundwa na Wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara ni Donald Msula, Ramadhan Makala, Mwasubila Japhet, Miraji Makala, Ally Omary Kasim Mkude, Paulo Kokolo na Dismas Ngeresha, ambao wote waliandikiwa barua za Utambulisho na Mtendaji Dego,hivyo  wananchi wanawashangaa Mtendaji na Mwenyekiti Mathias kuwakataa baadhi ya wajumbe kwa itikadi za kisiasa.
 
Awali wananchi watatu Salum Mzimba, Hilal Fungo na Fikiri Mahugu waliwashitaki viongozi wa Halmashauri ya kijiji hicho akiwemo Mwenyekiti Mathias kwa kupora, kuvamia na kujenga nyumba kwenye maeneo ya shule hizo, ambapo kesi Na. 70/2011 iliyopelekwa Baraza la Ardhi la Katay a Diongoya ya Agosti 11, 2012 ilitupilia mbali madai hayo, lakini wanapinga uamuzi huo kuwa una kasoro.

No comments:

Post a Comment

Pages