April 02, 2013

WANANCHI KILIMAHEWA WALIA UVAMIZI WA ENEO LAO


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Salasala, Abdallah Mpondela akionesha eneo la wazi la serikali ambalo hutumiwa na wananchi wa eneo hilo kwa ajili ya michezo mbalimbali pamoja na shughuli za kijamii. Eneo hilo kwa sasa limevamiwa na mtu asiyefahamika anayedai kuwa ndie mmiliki wa kiwanja hicho ambacho kina  Ofisi ya Mtaa na Kata. (Na Mpiga Picha Wetu)
Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa.

DAR ES SALAAM, Tanzania

WANANCHI wa Mtaa wa Kilimahewa Kata ya Salasala wamemtaka Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuingilia kati mgogoro wa kiwanja cha wazi cha serikali.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilimahewa Abdallah Mpondela alisema kuwa kiwanja hicho kimeingia katika mgogoro na mtu ambaye hafahamiki na kusema ndio mmiliki wa kiwanja hicho kukiwa kuna ofisi ya Mtaa pamoja na ofisi ya Kata hiyo.

Mpondela alisema kuwa mtu huyo ambaye anasema kiwanja hicho ni mali yake huku Manispaa ya Kinondoni imejenga ofisi katika eneo hilo ambapo katika ramani inaonyesha ni mali ya serikali.

Mwenyekiti pamoja na wananchi wamesema kuwa hawataweza kuachia kiwanja hicho kwenda katika mikono ya mtu mwingine kwa masilahi yake huku wakinanchi wakikosa eneo hilo linalotumika katika michezo na mikutano mikubwa.

Mpondela alisema kuwa mtu huyo alifikia kwenda mahakamani kwa kumshitaki Mwenyekiti wa Mtaa ambapo hajaweza kifika kizimbani kusimama katika kudai hicho kiwanja kuwa ni mali yake tangu ilipofunguliwa kesi na mtu huyo.

Wakili wa Kujitegemea wa Kutetea kiwanja hicho upande wa Mwenyekiti wa Kilimahewa Addo Mwasongwe alisema kuwa atahakikisha kiwanja hicho kinabaki katika mikono ya wananchi kwa shughuli za kijamii.

Mwasongwe alisema kuwa kazi yake ni kuona haki inatendeka kwa wananchi wa Kilimahewa kuenndeka kumiliki eneo hilo kutokana na ramani inavyoonyesha kuwa eneo la wazi la serikali.

No comments:

Post a Comment

Pages