HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 13, 2013

Serikali iingilie Mahakama Zisiwafanye Wananchi Wasifanye Kazi

Na Bryceson Mathias
UTAKAFITI nilioufanywa katika Mahahakama mbalimbali nchini, Ucheleweshaji wa Kesi na kutokuwepo kwa Taarifa Mahususi kuhusu kutohukumiwa kwa kesi, kunawafanya wananchi kupoteza muda wa kufanya kazi za kuwapatia maendeleo ya Taifa na za manufaa yao.
Hakimu anaweza kuwa na Kesi kwa uchache 10, na wote akawapangia kufika siku, saa na tarehe moja (saa 2.30 asubuhi kwa mfano), kwa upana na urefu wa kusikiliza, kesi tatu zikamfikisha saa za kufunga Mahakama, hivyo watu saba (7), wanakuwa wamepoteza Muda.
Lakini kama Mahakama kupitia Serikali Kuu kwa kutumia Teknolojia ya Digitali, ingeweza kuwapunguzia wananchi usumbufu, kwa kuwapangia muda kwamba kesi ya Kwanza itasikilizwa kwa Masaa Matatu kwa Mfano, Mtu wa pili angeambiwa aje saa 5.00 ili azalishe mali.
Mwenye kesi ya Tatu angetakiwa afike saa 7.30, na kama kuna dharura Hakimu hayupo basi ni vema Mteja akaarifiwa kwa simu asifike, kuliko mtu akafika na kukaa bila kesi kusilizwa na baadaye anaambiwa Hakimu Hayupo tunaahirisha kesi, wakati muda huo angefanya Kazi.
Kama Mahakama inafahamu kuwa mfanyakazi wake (Hakimu), ameomba ruhusa hayupo kutoka na Dharura, kuliko kumsumbua mtu atoke Sumbawanga, Kigoma au Mtwara, asumbuke hadi Dar es salaam, halafu akifika Mahakamani ndipo anaambiwa kuahirishwa ni mbaya.
Si kila mwananchi ana uwezo wengine hata nauli wanakopa, hivyo Mahakama kupitia Serikali, zikijihamisha kutoka kwenye Analogia na kuhamia Digitali, katika Shughuli zao za Ki-Mahakanaka, wananchi watapata nafasi ya kuzalisha Mali na maendeleo yao.
Hali hii inaweza kuisaidia Serikali, Mahakama na Wateja, kuepuka Gharama zisizo za lazima, ambazo kimsingi zingeepukwa kwa mfano Gharama za Shajala (Stationery), Muda wa Kazi wa Ziada (Overtimes), Gharama za Usafiri kwa Wafungwa (Transport Cost-Mafuta) nk.
Lakini pia ingeweza kupunguza, usumbufu kwa watendaji wa Mahakama kama Polisi, Askari wa Magereza na wafungwa wenyewe, ambapo kwa upande mwingine ingeepusha Madhara kama bahati mbaya ingeweza kutokea ajali, wafungwa na watendaji wangeweza kuathirika.
Washwahili wanasema, ‘Haraka haraka haina Baraka’. Kwa upande mwingine, badala ya kesi kuhukumiwa kwa kwa haraka haraka bila na kujichosha (Monotonous) bila kuzama na kubaini  viini halisi vya tatizo, watendaji hao watakuwa na Muda muafaka kutoa Haki stahili.
Nasema hivyo kwa sababu, ni kawaida mtu akifanya kazi nyingi kwa kurudia rudia bila kupumzika, mambo Matatu huwa yanakosekana (SAD); Usalama (Security), Usahihi (Accuracy) na Nidhamu ya Kazi (Discipline.
Kutokana na Mpangilio mzuri wa utendaji wa kuhukumu Kesi kiutaratibu, Malalamiko yanayotolewa na wananchi kwamba, Kesi zinacheleweshwa na kuilaumu Serikali na Watendaji wake, kutoa tuhuma za Rushwa zingepungua kwa sababu adhaa hiyo isingeonekana kirahisi.
Aidha ili kupima ufanisi wa watendaji wa Mahakama, ni vema kama ungewekwa utaratibu kwamba, Kila Hakimu anatakiwa kuhukumu Kesi ngapi kwa siku, Wiki, Mwezi na hata Mwaka. Na kama ufanisi huo haukufikiwa, basi pawepo hatua za Msingi kusukuma Gurudumu hilo.
Iwapo tunamtaka Mzalishaji Mali Kiwandani afikishe Tani Kadhaa, na Mkulima alime Kitalaamu na kupata Gunia Kadhaa, na Mfugaji afuge Kitalaam; basi hata Hakimuu lazima tumuwekee viwango vya kutenda Kazi ili ufanisi wake uonekane na kupimwa.
Uahirishwaji wa Kesi nyingi kwa mfululizo, ndio unaosababisha Mlundikano wa Kesi hizo, ambapo baadaye huibua malalamiko, na katika Mabaraza ya Kata wananchi waawekewe wansheria wa kuwasaidia.

No comments:

Post a Comment

Pages