September 16, 2013

ALLY NIPISHE AISAMBZA 'KWEA PIPA BINADAMU'

Na Elizabeth John

MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Ally Nipishe, anatarajiwa kusambaza ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kwea pipa binadamu’, hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ally Nipishe alisema anashukuru wimbo wake wa ‘My’ umekubalika na amekuwa akipata shoo mbalimbali ndani ya Dar es Salaam, katika kazi hiyo kamshirikisha mkali wa muziki wa mduara nchini, Ally Ramadhan ‘AT’.

“Nashukuru Mungu kwamba toka nimetoa wimbo wangu wa ‘My’ unaendelea kufanya vizuri, umekubalika kwa haraka kwa sababu nimetoa ujumbe ambao ni wa kuelimisha jamii, pia napata shoo,” alisema.

Ally Nipishe alisema, baada ya kuusambaza ‘Nikupulike’, ambao umeanza kufanya vizuri katika redio mbalimbali, anajipanga kusambaza video yake kabla ya kuisambaza ngoma hiyo mpya.


 Msanii huyu kipaji chake kilianza kuvuma pale aliposhirikishwa na msanii wa kike, Mwasiti, katika kazi yao inayokwenda kwa jina la ‘Ni Wewe’, ambako alionekana kufanya vizuri na mashabiki kumtaka atoke na wimbo wake.

No comments:

Post a Comment

Pages