September 13, 2013

CRDB BANK YAZIDI KUFUNGUA FURSA KATI YA TANZANIA NA CHINA

 Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB wakisoma vipeperushi vyenye taarifa za huduma mbalimbali za benki hiyo wakati wa maonesho ya bidhaa za China yanayofanyika Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa benki hiyo anayesimamia Dawati la China, Ibrahim Masahi.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Kitengo cha Dawati la China, Ibrahim Masahi akitoa ufafanuzi kuhusu huduma wanazotoka kwa raia wa China wakati wa maonesho ya bidhaa za China.  
Watu mbalimbali waliojitokeza katika maonesho hayo wakipata maelezo huduma za kibenki katika banda la benki ya CRDB.
Ofisa Masoko wa benki ya CRDB, Gerald Mhalanyambu (kulia), akitoa maelezo ya huduma wanazotoa kwa baadhi ya watu waliotembelea banda lao.
Wateja wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na benki ya CRDB.

DAR ES SALAAM, Tanzania

HUDUMA ya Dawati la China katika Benki ya CRDB imepata mafanikio makubwa kwa kuchangamkiwa na wateja wengi tangu ilipozinduliwa rasmi Machi 27, mwaka huu.
Kuwasaidia wafanyabiashara wa Tanzania wanokwenda China

Akizungumza katika banda la CRDB kwenye Maonyesho ya Biashara ya China, Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam,

leo, Meneja Mahusiano anayesimamia dawati la China, Ibrahim Masahi alisema, zaidi ya fedha za China Yuan milioni

55 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 14.3 zimeweza kubadilishwa kupitia huduma ya dawati hilo.

Masahi alisema, tangu huduma hiyo izinduliwe CRDB imepata ongezeko la asilimia 70 ya wateja, wanaotumia huduma

hiyo ambao ni Watanzania wanaokwenda China au Wachina wanaokuja Tanzania kwa ajili ya shughuli za biashara au

matembezi.

Alisema, kupitia dawati hilo, kuna kuna huduma ya UnionPay ambayo ni sawa na Master Card au Visa Card

zinazomwezesha mteja kutoka Tanzania kuchukua fedha kwenye ATM ya benki yoyote akiwa nchini China, kadhalika

inamwezesha pia anayetoka China kuchukua fedha kwenye ITM za CRDB akiwa Tanzania.

Masahi alisema, ili kuboresha huduma hiyo ya Dawati la China, CRDB imeweka mahusiano ya kibishara na Benki mbili

nchini China ambazo ni Bank Of China HBC ya Beijing nchini humo kwa ajili ya huduma ya kusafirisha fedha kiwa

haraka zaidi kutoka Tanzania kwenda huko.

"Kama siyo tofauti ya muda kati ya Tanzania na China, wateja wetu wangekuwa wanapata fedha ndani ya saa 24, hata

hivyo haiichukui muda mrefu mtenja aliyeko China kupata fedha tunayomtumia kutoka hapa Tanzania", alisema

Masahi.

Maonyesho hayo ya aina yake, ambayo yalifunguliwa jana, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, yanashirikisha kampuni zaidi

ya 100 kutoka China ambazo zinaonyesha bidhaa mbalimbali zikiwemo za nyumbani na za kiteknolojia.

No comments:

Post a Comment

Pages