September 22, 2013

Je Serikali ni Chanzo cha kukithiri Wahamiaji Haramu?

Na Bryceson Mathias
KUTOKANA na Serikali kutafsirika kuwa inapuuza Michango ya Wabunge kuhusu Wimbi la Wahamiaji Haramu nchini na hasa michango ya Upinzani, sasa Serikali imekurupuka na kukumbuka Shuka dhidi ya wahamiaji hao, wakati kumekucha.
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Morogoro,Suzan Kiwanga,alimvaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuhusu wahamiaji waliojificha kwenye Viwanda mkoani humo.
Sheria ya Uwekezaji inataka Uwekezaji kuajiri Watalaam Wageni watano tu, lakini sasa wamerundikana zaidi ya 10 hadi 20 viwandani hasa vya Sukari kama Kilombero, Mtibwa, Kagera na TPC-Arusha, jambo linalotafsirika Serikali ndiyo Chanzo cha Wahamiaji Haramu.
Ingawa Serikali imeanza Oporesheni Kimbunga kuwasaka Wahamiaji hao, bado inaonekana kuchagua na kuyaacha maeneo muhimu kama viwanda tajwa vya Sukari, na mashambani ambapo huja na wake zao au waume zao ambao nao hutafutiwa kazi kinyemela bila vibali.
Kimsingi kazi wanazopewa hawazijui na badala yake huwa wanafundishwa na wazawa na cha kusikitisha utaona wanalipwa mishara mikubwa na marupurupu mara tano zaidi ya wazawa waliowafundisha kazi.
Katika Kiwanda cha Sukari Mtibwa kwa Mfano; unakuta Mwanaume anakuja toka Ufilipino na mkewe na Mtoto, rafiki yake wa kike ambaye naye atatafutiwa kazi kinyemela ambazo wazawa wanaweza kuzifanya hivyo badala ya watalaam watano, sasa wanakuwa 10-15.
Hivi karibuni mtibwa walinaswa wageni hao zaidi ya 10 wakiwa hawana vibali vya kuishi nchini, lakini wenzetu wa uhamiaji sijui walilichukua kwa mtindo upi lakini jambo hilo lilifunikwa funikwa hakuna picha halisi ya tua zilizochukuliwa.
Nakumbuka siku za Nyuma Mtibwa waliwahi kumwagwa wachomeaji wa Vyuma zaidi ya 20 kiwandani hapo kufanya kazi hiyo ambao nguvu kazi ya watanzania ingeweza kufanya kwa umahiri mzuri kuliko wao ambao walionekana wanafundishwa tu!
Mbunge Kiwanga, alipohojiana na Mwandishi juu ya Hoja na Ushauri wake wa Wahamiaji haramu kama unapuuzwa na Dk. Nchimbi alisema; Hali ya Mtibwa ilivyo, ndiyo ilivyo kwenye Kiwanda cha Sukari Kilombero na maeneo mengine nchini hasa mkoani kwake Morogoro.
Alisema, wakati Serikali inahangaika na Wahamiaji mikoa ya mipakani ikiwakamata walalahoi wanaotuhumiwa kuwahifadhi, bado haijawakamata vigogo wanaofadhiri na kujipatia fedha Lukuki kuhifadhiwa kwa Wahamiaji hao kwenye Viwanda vya Sukari na sehemu zingine mkoani Morogoro.
Mbali ya Kiwanga kulalamikia uwepo wa wahamiaji hao kiholela Morogoro, Mfanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa alisema, kiwandani kwao kuwepo kwa Wahamiaji haramu (Wageni) zaidi ya 10 ni jambo la kawaida akidai, huko mbeleni uwingi wao utawazidi wazawa.
Aligusia mfano wa Wimbi la Wachina kujaa jijini Dar es Salaam wakiuza vitu vya kawaida Juice, Nguo, Dawa za asili za Kichina na kuisema kwa sasa wameeanza kuenea kila Wilaya na  Mikoa na alieekeza kuwa, kwa sasa wamevamia hadi Mji Mkuu Dodoma.
Alisema, wanatafsiri labda fadhira hiyo ndiyo iliyomkuna Balaozi wa Uchina kufikia kujisahau na kushabikia Chama Tawala (CCM) kwa kule kukumbatiwa kwa watu wake wafanye biashara yoyote nchini, Ukandarasi, Uuzaji wa Matunda, Dawa na Pikipiki akisema baadae watajaa na nchi hii itakuwa kama yao.
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, pamoja na Urafiki Mzuri na China enzi za Mao, hakukubali wala kuthubutu kuwamwaga wachina nchini ijapokuwa kulikuwa na Miradi ya pamoja, Viwanda vya Urafiki, Reli ya TAZARA na mengi mingineyoInashangaza sasa! Tumelogwa na nini?
Aidha enzi ya Nyerere hatukuona watoto wa asili hizo lakini leo tunashuhudia watoto wengi wanazaliwa na watanzania wenye Jamii hiyo, Vijijini na Mijini. Je. Tunakwenda wapi kama si kufirisiwa na kupokwa kwa nchi yetu?
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308.
 

No comments:

Post a Comment

Pages