September 16, 2013

JINA LA WIMBO LAMUUMIZA KICHWA SUMA LEE



Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail Seif ‘Suma Lee’ anajipanga kuachia kazi yake mpya hivi karibuni ambayo bado hajaipatia jina kutokana na ubora wa kazi hiyo.

Suma Lee alishawahi kutamba na kazi zake kama, ‘Utanikumbuka’, ‘Hakunaga’, ‘Chungwa’ na nyinginezo ambzao zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini.

Kwa mujibu wa Suma Lee, kazi hiyo ameshaindaa kilichobaki ni kuipa jina na kuisambaza katika vituo mbalimbali vya redio.

“Nashindwa niipe jina gani hazi hii kutokana na ubora ulionao nimejaribu kuwashirikisha wasanii wenzangu wanisaidie lakini kila mmoja anaupa jina lake, tutakubalina na kuchagua lililo bora zaidi,” alisema.

Alisema anaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo ambayo anaamini ataisambaza ikiwa pamoja na video yake ili kuwapa burudani iliyokamilika mashabiki na wapenzi wa kazi zake.

No comments:

Post a Comment

Pages