September 14, 2013

KIVUMBI LIGI KUU YA ENGLAND KUENDELEA LEO


LONDON, England

Mabingwa watetezi, Manchester United watakuwa nyumbani Old Trafford, kuwaalika Crystal Palace, katika mechi ya mapema, itakayofuatiwa na nyingine sita tofauti kwenye viwanja vya Villa Park, White Hart Lane, KC, Britania, Light na Craven Coattage

BAADA ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, timu 16 kati ya 20 za soka za Ligi Kuu ya hapa leo zinajitupa kwenye viwanja nane tofauti kuwania pointi muhimu.

Mabingwa watetezi, Manchester United watakuwa nyumbani Old Trafford, kuwaalika Crystal Palace, katika mechi ya mapema leo, itakayofuatiwa na mechi sita tofauti kwenye viwanja vya Villa Park, White Hart Lane, KC, Britania, Light na Craven Coattage.

Wenyeji wa dimba la Villa Park, Aston Vila watakuwa hapo kuwaalika Newcastle United, huku Tottenham ikiumana na Norwich City huko White Hart Lane jijini hapa, na Hull City ikitunishiana misuli na Cardiff City huko kwenye Uwanja wa KC.

Manchester City na Arsenal zina nafasi ya kupaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, kama zitaweza kuibuka na ushindi mnono kwenye viwanja vya ugenini, ambapo Man City itakuwa Britania kuwavaa wenyeji Stoke City, huku Arsenal ikiwa Light dhidi ya Sunderland.

Wenyeji wa Uwanja wa Craven Coattage, Fulham watakuwa nyumbani kuwaalika West Brom Albion, ambapo mechi ya mwisho kabisa jioni ya leo itakuwa baina ya Everton, watakaowakaribisha Chelsea, kwenye dimba la Goodison Park.

Vinara wa ligi hiyo kabla ya mechi za leo, Liverpool watakuwa mapumziko kwa muda zaidi hadi Jumatatu, watakaposafiri kuwafuata Swansea City kwenye dimba la Liberty, wakati kesho Jumapili, Southampton watawaalika West Ham kwenye Uwanja wa St Mary’s.

Ratiba mechi za leo Ligi Kuu ya England
Man Utd          v          Crystal Palace  - saa 8:45        
Aston Villa       v          Newcastle        - saa 11:00      
Tottenham        v          Norwich           - saa 11:00      
Hull                  v          Cardiff              - saa11:00       
Stoke               v          Man City          - saa 11:00      
Sunderland       v          Arsenal - saa 11:00      
Fulham v          West Brom       - saa 11:00      
Everton            v          Chelsea            - saa 1:30        


Supersport.com

No comments:

Post a Comment

Pages