Kipa wa Man United, David de Gea akimpiga kwa mikono miwili nahodha wa Man City, Vicent Kompany, katika jaribio la kuondosha hatari langoni kwake. Katika mechi hiyo Man City ikiwa nyumbani Etihad iliilaza Man Utd kwa mabao 4-1.
Mwamuzi (sio wa mechi hiyo) Graham Pool kulia, akizungumza na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya England, Jamie Redknapp na Martin Keown wakati wa mechi baina ya Man City na Man United kwenye Uwanja wa Etihad jana jioni, ambapo United ilichapwa kwa mabao 4-1.
Mwamuzi Howard Webb akimuonesha kadi ya njano nyota wa Man City Matija Nastasic kutokana mchezo mbaya.
Mshambuliaji Sergio Aguero (wa pili kulia), akiifungia Man City bao la uongozi katika mpambano huo, huku mabeki Nemanja Vidic na Patrice Evra na mlinda mlango wao David de Gea wakishuhudia.
Aguero akishangilia bao hilo, ambalo ni la 50 tangu alipojiunga na Man City.
Howard Webb akimuonesha kadi ya njano mshambuliaji Wayne Rooney wa Man United katika pambano hilo.
Kiungo Yaya Toure wa Manchester City (kulia) akifunga bao la pili la timu yake dhidi ya Man United.
Toure akishangilia bao hilo.
Aguero akiutazama mpira wake ukitinga nyavuni kumpita mlinda mlango De Gea kuiandikia Man City bao la tatu.
Aguero (wa pili kushoto) akishangilia pamoja na Alvaro Negredo na Samir Nasri.
Samir Nasri akiifungia Man City bao la 4 la Manchester City.
Nasri akishangilia bao hilo, huku beki wa Man Utd, Smalling akisikitikia kichapo hicho.
Wayne Rooney wa Man United (wa pili kulia), akiifungia timu yake bao la kufutia machozi kwa adhabu ndogo 'free kick.'
Wachezaji wa Man City wakipunga mikono kwa mashabiki kuwashukuru kwa sapoti yao baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi Howard Webb.
No comments:
Post a Comment