MWANADADA anayetamba katika muziki wa kizazi kipya nchini, Baby
Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la
‘Summer Holiday’ ambayo imeanza kubamba katika vituo mbalimbali vya redio ndani
na nje ya nchi.
Baby Madaha alishawahi kutamba na ngoma yake ya ‘Amour’ ambayo
ilifanya vizuri na kumtambulisha katika tasnia ya muziki huo.
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, Baby Madaha kasambaza ngoma hiyo
wiki iliyopita na tayari imeshaanza kubamba katika nchi mbalimbali kutokana na
ubora wa wimbo huo.
“Katika wimbo huo, naamini
nimefanya vizuri kutokana na mashairi ya wimbo huo kusimama pamoja na ubora wa
kampuni ambayo nimeifanyia kazi hiyo, naomba wapenzi wa kazi zangu wanipokee
kivingine zaidi,” alisema.
Baby Madaha aliwataka
mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake na kwamba kuna vitu
vingi ambavyo amewaandalia, wasicheze mbali na yeye.
No comments:
Post a Comment