September 11, 2013

Wakulima;Ng’ombe 1,000 kutozwa Sh.50,000/- kila mmoja?

Na Bryceson Mathias, Sungaji Mvomero
NG’OMBE zaidi 1,000 huenda wakatozwa faini ya sh. 50,000/- kila mmoja, baada ya walinzi wa Jadi wa Kijiji cha Kisala Kata ya Sunguji, kukamata Ng’ombe hao waliongizwa mashambani na kula mazao, ambapo wakulima wametaka kila Ng’ombe atozwe faini ya Sh. 50,000/- la sivyo hakitaeleweka.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kikundi cha ulinzi cha wakulima kilichoundwa kwa nia ya kuhami mazao yao dhidi ya mifugo ya wafugaji, kukamata Ng’ombe hao ikiwa ni siku chache baada ya Mkuu wa Wilaya, Antony Mtaka, kunusuru mapigano baina yao.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kisala, Shija Msafiri, amethibitisha Walinzi wa Jadi waliopata mafunzo maalum kijijini hapo toka kwa Waijaki wa Ukaguru, kuwa wamekamata Ng’ombe hao zaidi ya 1,000,000/- na wanawadhibiti.
“Ng’ombe hawa wamethibitiwa hapa na wakulima, na wanataka Sheria Ndogo ya Serikali za Mitaa inayokataza kuingiiza mifugo mashambani kwa jinai ichukue mkondo wake, hivyo kila Ng’ombe anastahili kulipiwa faini ya Shilingi 50,000/- la sivyo hakieleweki kitu“. alisema Shija.
Mlinzi wa wa Amani na Mtendaji wa Kata ya Sungaji, Elizabeth Mgaya, alipohojiwa awali alionesha kumpuuza Mwandishi akidai hawezi kutoa taarifa kwake, alipobanwa kuwa tabia ya kuhodhi taarifa ndiyo inayowafanya wakulima waone kama wanakula rushwa akajibu!.
“Ni kweli Ng’ombe hao wamekamatwa  wakiwa na Mchungaji mmoja, lakini tunaamini kundi  hili haliwezi kuwa la mtu mmoja, hivyo tunangoja kuwakamate wahusika wengine ili  tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria”.alisema Mgaya huku akikwepa kama watatozwa Sh. 50,000/- kila Ng’ombe au laa!.
Aidha hivi karibuni Mkuuu wa Wilaya ya Mvomero Mtaka, alitoa siku saba kwa wafugaji waliovamia makazi ya wakulima wilayani humo, kuhama kwa hiari yao na siku 14 za kuhamishwa kwa Nguvu, lakini wafugaji hao wanaonekana kupuuza amri ya Mtaka, na hivyo wameendelea kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kwa makusudi.
  

No comments:

Post a Comment

Pages