December 30, 2013

SHUKURANI TOKA KWA FAMILIA YA MRUMA

Familia ya Mruma ya Dar es Salaam na Ugweno, Mwanga inatoa shukurani nyingi
kwa ndugu,jamaa,marafiki, majirani na Watanzania wote waliojitokeza kuwa
nao kwa njia tofauti katika kipindi cha msiba wa mtoto wao mpendwa Jerry
ambaye alifariki dunia Nairobi tarehe 17 Novemba na kuzikwa Dar es Salaam
tarehe 26 Novemba 2013.



Ni vigumu kutoa shukurani hizi kwa majina. Kwa njia ya kipekee, tunaomba
tuwataje wachache kwa niaba ya wote kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Balozi wa Tanzania Kenya Mh. Dr. Batilda Burian na wafanyakazi
wa ubalozi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya magazeti ya Serikali ( Daily News na
Habari Leo); Uongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha USIU, Nairobi; Lee
Funeral Home, Nairobi; Bwana na Bibi Mutinda wa Athi River, Nairobi; Bwana
na Bibi Ouma wa Kitengela, Nairobi; Hoteli ya Ololoitikoshi
Resort, Kitengela; Mchungaji Kiongozi na wazee wa Usharika wa Mbezi Beach
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jumuiya ya Betheli,
Mbezi Beach; Mheshimiwa CD Msuya; Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Afrika
Mashariki - Mh. Angela Kizigha, Mh. Nderakindo Kessy, Mh.Shyrose Bhanji,
Bwana na Bibi Kachenje wa Mbezi Beach; Swissport Dar es Salaam; Qnet
Kenya; Love Titans - Nairobi, Kenya; Kibosho Girls Reunion, Mbezi Beach Family.

 
Katika kipindi kama hiki ni rahisi kuishiwa na maneno ya kuelezea faraja
tuliyopata kwa namna mlivyokuwa nasi wakati wote na pia mlivyotuombea.
Maneno pekee yanayokuja haraka ni AHSANTENI SANA, MUNGU AENDELEE
KUWABARIKI.









No comments:

Post a Comment

Pages