December 26, 2013

SOLLY MAHLANGU ATIKISA TAMASHA LA KRISMASI DAR, LEO KURINDIMA MOROGORO
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka afrika Kusini, Solly Mahlangu (katikati) akicheza na mashabiki wake wakati wa tamasha la Krismasi lililofanyika kweny uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Solly akiwajibiki jukwaani.

Anitha Kijambula akiimba nyimbo ya Solly wakati wa tamasha hilo.
Tumaini Ntobo.
Kundi la The Voice likitumbuiza.
Mather Oliver akionesha umahiri wake.
Umati wa mashabiki uliojitokeza katika tamasha hilo.
Sarah Mvungi naye akuwa nyumba.
Edson Mwasabwite akiimba.
 Tito Jackson akipokea zawadi ya CD kutoka wa Solly baada ya kucheza vizuri nyimbo za msanii huyo.
 Solly Mahlangu akimtambulisha mke wake.


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu Bunge), Williamu Lukuvi, amewataka waimbaji wa nyimbo za Injili, kuiombea nchi iendelee kuwa katika amani, ili kila mmoja aweze kufanyakazi zake bila hofu.

Lukuvi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana,  wakati wa Tamasha la Christmas 2013 lilliloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion.

Alisema pamoja na hayo, bado serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika  kupigania amani ili kudumisha mshikamano uliyojengeka kwa muda mrefu.

“Tunamuomba mungu andelee kuiweka nchi katika amani ambayo itawafanya muendelee kuwa huru, kuitangaza injili pia kuitangaza nje ya nchi.

“Namshukuru Msama kwa kutukutanisha katika tamasha hili ambalo kwa mwaka huu ni la pili baada ya lile la Pasaka, napongeza na kumtaka aendelee kuandaa matamasha hayo, ambako hata serikali inatambua nyimbo hizo za Injili, ndio maana nilikubali kushiriki tamasha hili.
Aidha, waimbaji wa tamasha hilo walikuwa ni Bony Mwaitege, Rose Mhando, Edson Mwasabwite, Upendo Nkone, Upendo Kilahilo, John Lisu, New Life Band na The Voice Acappella.

Wengine wa kutoaka nje ni Solly Mahlangu, Liliane Kabaganza na Ephraim Sekeleti ambako waimbaiji Mwaitege, Mhando na Mahlangu walioneka kushangiliwa zaidi.

Mahlangu paboja na kutoa burudani pia aliitumia siku ya jana kusherehekea siku ya kuzaliwa mke wake ambapo aliamua kufanya hivyo kwa ajili kuheshimu mwaliko wa kuja Tanzania kwani bila hivyo angeamuwa kubaki nyumbani kufanya sherehe hiyo ya mkewe.

Msama alimshukuru Waziri, Lukuvi kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwani ni mara chache kwa baadhi ya viongozi kukubali kuhudhuria sherehe kama hizo kwa madai ya kuwa na kazi nyingine.

Aliongeza kuwa tamasha hilo lingendelea jana mkoani Morogoro, kisha litahamia Tanga na kumalizia Arusha.

No comments:

Post a Comment

Pages