MKALI wa muziki wa taratibu ‘RnB’ nchini, Bernad
Poul ‘Ben Pol’, amesema malengo yake katika tasnia hiyo ni kufanya kazi na
wasanii wa kimataifa ili kukuza muziki huo kwa wadau na wapenzi wake.
Baadhi ya wasanii ambao Ben Pol amesema
anatamani kufanya nao kazi ni kama, Peter na Paul Okoye ‘P.Square’, Martin
Justice 'J.Martin', Kundi la Brackets, Timaya Ukwu 'Timaya' na wengine ambao
wanafanya vizuri katika Bara la Afrika.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Ben Pol alisema hiyo ni mipango yake ambayo anataka kuitimiza ndani ya mwaka
huu baada ya kufanya vizuri mwaka uliopita.
Alisema mwaka jana ulikuwa ni mwaka wa mafanikio
kwake, hivyo anataka kuendeleza mashambulizi kwa kufanya kazi na wasanii wa
kimataifa na kuhakikisha anawashika mashabiki wengi tofauti na miaka iliyopita.
“Nina mipango ya kuboresha muziki wangu, kwa
kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa napenda kuanza na wasanii wa Nigeria, kutokana
na ukaribu ambao nipo nao kwasasa hivi, nikifanikiwa na hao itanibidi nizunguke
katika nchi nyingine, hii yote ni kutaka kutimiza malengo yangu ya kuwa
mwanamuziki mkubwa na kukubalika nchi zote za Duniani,” alisema Ben Pol.
No comments:
Post a Comment