January 05, 2014

MAELFU WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA DK. WILLIAM MGIMWA LEO
 Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa wakati ulipokuwa ukiwasili leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Maziko ya marehemu Mgimwa yatafanyika Jumatatu kijijini kwake, Magunga mkoani Iringa. (Picha zote na Francis  Dande)
 Rais kikwete wakati akiwasili.
Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha marehemu Dk. William Mgimwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo. Dk. Mgimwa atazikwa Jumatatu Kijijini kwake Magunga Mkoani Iringa. 
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho.
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimfariji  mjane wa marehemu Dk. William Mgimwa,  Jane Mgimwa wakati wa kuaga mwili katika viwanja vya Karimjee.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa waziri wa Fedha, marehemu Wiliam Mgimwa katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha marehemu Dk. William Mgimwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam 
Mama Maria Nyerere akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Aliyekuwa waziri wa Fedha na Uchumi. Dk. William Mgimwa Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba wakati wa kuaga mwili wa Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi. Dk. William Mgimwa.
 Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Aliyekuwa waziri wa Fedha na Uchumi. Dk. William Mgimwa Dar es Salaam.
 Dk. Bilala akiifariji familia ya aliyekuwa waziri wa fedha na Uchumi, marehemu Dk. William Mgimwa.
 Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima za mwisho.
 Mabalozi wanaowakilisha nchi zao wakitoa heshima za mwisho.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msururu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
Rais Kikwete akitoa pole kwa familia ya marehemu aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya akifuta machozi baada ya kushindwa kujizuia wakati akisoma wasifu wa marehemu Dk. William Mgimwa katika viwanja vya Karimjee dar es Salaam jana, wakati wa kuaga mwili. Dk,. Mgimwa atazikwa leo Kijijini kwake Magunga Mkoani Iringa

No comments:

Post a Comment

Pages