January 25, 2014

MKUTANO MKUU WA NGUMI ZAKULIPWA WAJA
FEBRUARI mosi katika ukumbi wa vijana hall kinondoni kutakuwa na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi wote ulioitishwa na orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa lengo la kuwakutanisha mapromota wote, mabondia na makocha  wa ngumi wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa. 

Aidha mkutano huo utatoa fursa ya kuelimishana sheria za ngumi za kulipwa  zinavyotumika kinyume na sasa, sheria nyingi zinafumbiwa macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi nchini. 
 Mkutano huo ulioitishwa na Rais wa TPBO,  Yasin Abdallah akishirikiana  na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili wa kitwe Traders unatarajiwa  kuwa mkutano wa kwanza  kuwakutanisha mapromota wote pamoja na mabondia wa ngumi  za kulipwa wa hapa nchini.

Ili kuboresha ngumi na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze kuudhamini mchezo huo, ambao ndio mchezo unaoliletea mataji na  sifa Tanzania katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini  wowote ,mpaka sasa ni mchezo  ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za  wadau wachache wachovu  na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni mchezo  ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini ili  uendelee kuboreka zaidi.


Akizungumza na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe, amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel mlundwa,names kavishe,  makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli,  matumla, Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau wa karibu na ngumi wamealikwa kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya terehe moja ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe alimaliza kwa kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa na promota wangumi  ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu sana kwa wamasumbwi ya nchi  yetu.

No comments:

Post a Comment

Pages