January 28, 2014

MPIGA TUMBA MAHIRI WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA
Mpiga Tumba mahiri wa The African Stars 'Twanga Pepeta', Soud Mohamed 'MCD' amefariki dunia Mkoani Kilimanjaro. 
Kwa mujibu wa msemaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Hassan Rehani alisema kuwa taarifa zaidi zitatolewa baadae.
'MCD alikua Moshi kwa ajili ya matibabu maradhi ya Kifua Kikuu na kuendelea na matibabu kwa zaidi ya miezi miwili na hali yake iliendelea vizuri hadi usiku wa Januari 27 hali yake ilipobadilika na kufariki dunia' 
Bendi alizowahi kuzipigia MCD, enzi ya uhai wake ni pamoja na Diamond Sound, Mashujaa Band na Twanga pepeta.

No comments:

Post a Comment

Pages