Madiwani wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kushoto) kukata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika Shule za msingi katika Kata 13 za jimbo hilo. Hafla hiyo imefanyika leo Chuo cha Ufundi Chang'ombe, Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza baada ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika shule zilizopo katika Kata 13 za Jimbo hilo. Madawati hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo yalikabidhiwa kwa madiwani wa Kata hizo katika hafla iliyofanyika Chuo cha Ufundi Chang'ombe, Dar es Salaam
Naibu Meya wa wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga akitoa shukurani kwa Mbunge Mtemvu kutoa madawati hayo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Zena Mgaya akimpongeza Mtemvu kwa juhudi za kuinua kiwango cha elimu wilayani Temeke.
Ofisa Elimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba akieleze furaha ya kupata madawati hao 500 yatakayopunguza tatizo la madawati wilayani Temeke.
Mtemvu akiangalia wakati mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi akiandika jina lake.
mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi, akitoa shukurani kwa Mtemvu kwa niaba ya wanafunzi kwa kuwapatia madawati hayo
Fundi akiendelea kupiga msasa baadhi ya madawati hayo yalitotengenezwa VETA Chang'ombe
No comments:
Post a Comment