January 31, 2014

Mwizi wa Bodaboda achomwa moto na Kufa

Na Bryceson Mathias, Lusanga Mvomero

Wananchi wenye Hasira wa Kijiji cha Lusanga Gulioni, Jana Januari 30, wamelichoma Moto hadi kufa, Jambazi Sugu la Kata ya Kibati wilayani Mvomero linalojihusisha na Wizi wa Pikipiki, baada ya kutuhumiwa kuiba Pikipiki T581 CPT ya Mkazi wa Kunke Kata ya Mtibwa, Josia Pascal Luaga.
Jambazi hilo, ni miongoni mwa majambazi ya wizi wa pikipiki yaliyouawa na wananchi wa eneo hilo, ambayo yalikuwa yanasakwa na Polisi wilayani Mvomero, kufuatia kuwepo kwa wimbi la wizi wa bodaboda na unyang’anyi wa mali za watu uliokithiri katika Kata ya Kibati na kusababisha taharuki.
Akizungumza na gazeti hili alivyoporwa pikipiki na Igo, Luaga alisema, “Jumatano majira ya saa 2.30 usiku eneo la Kilimanyege barabara ya Maboi Mtibwa, kando ya Mfereji walijitokea watu watatu na kuweka Gogo kubwa ghala, lililomsababisha kuanguka na pikipiki.
“Nilipoamka mmoja wao akaanza kunifukuza na Panga ili anikate, lakini namshukuru Mungu nilimudu kukimbia, wakanipora bodaboda yangu na kufanikiwa kutoweka nayo, pamoja na simu yangu ya Line mbili”.alisema Luaga.
Luaga alidai, Siku ya pili Majambazi hao, walitumia simu yake (Luaga) kummpiga simu mdogo wake baada kuona namba zake kwenye simu, na kumwambia mwambia kaka yako aje achukue pikipiki yake kwa masharti ya kuwapa Sh. Laki 3/- kwa kuwatumia kwenye Airtel-Pesa.
Alisema, alifanikiwa kupata Sh. Laki 2/-, na nilikuwa nikiwatafuta kupitia namba hiyo baada ya kuwatumia fedha, wakawa hawapatikani, hadi alipofuatwa na waendesha bodaboda wenzake 30 wakisema, inaaminika Igo ameonekana Lusanga hivyo waongozane kwenda kumsaka, lakini wakakuta amechomwa.
Miongoni mwa waliotuhumiwa kuhusika katika wizi huo wakiwa na Igo, ni pamoja na Joseah Sadeki Mgaya na Mtu Moja aliyejulikana kwa Jina Moja la, Bariki Mkazi wa Mji Mdogo wa Madizini, ambao Polisi Turiani, imekiri kuwashikilia kwa mahojiano, wakiwa wamenusurika kuawawa kwa kipigo kikali,
Katika hali ya kushangaza, wananchi wa Kata ya Kibati na wale wa Kijiji cha Lusanga, Kunke, Bwagala na Mtibwa, wamesema wamefurahishwa na kuawa kwa Jambazi hilo, na kwamba hizo ni salamu kwa majambazi wengine wa wizi wa aina yoyote.

No comments:

Post a Comment

Pages