January 19, 2014

PSPF KWA KUSHIRIKIANA NA FLAVIANA MATATA FOUNDATION WAKABIDHI VIFAA VYA SHULE KISARAWE
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani wakifurahia zawadi za madaftari pamoja na mabegi vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa kushirikiana taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kuwasadia watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoni humo. Katikati ni mwanzilishi wa taasisi hiyo, Flaviana Matata. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Kisarawe, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande) 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Kimanzichana iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani, Kulwa Kijangwa  akipokea msaada wa vifaa vya shule kutoka kwa Ofisa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Hawa Kikeke uliotolewa kwa kushirikiana na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kuwasadia watoto wanaoishi katika mazingira magumu humo. Katikati ni mwanzilishi wa taasisi hiyo, Flaviana Matata. Hafla hiyo ilifanyika wilayani Kisarawe, mwishoni mwa wiki. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani wakicheza ngojela mbele ya wageni wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya shuleni hapo.
Wapigapicha wakiwa kazini.
Mwanamitindo Flaviana Matata akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Chanzige ambao  wanaoishi katika mazingira magumu wilayani Kisarawe. Taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kushirikiana na PSPF walikabidhi vifaa mbalimbali vya shule kwa ajili ya watoto hao.

No comments:

Post a Comment

Pages