January 20, 2014

TAARIFA YA  MSIBA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF, anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw Philemon Minga kilichotokea usiku wa tarehe 19 January 2014 nyumbani kwake Mwenge mjini Dar es salaam.

Mfuko unaendelea na taratibu za mazishi kwa kushirikiana na familia ya marehemu na mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatano tarehe 22 Januari 2014
Bwana alitoa Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe

Amina

No comments:

Post a Comment

Pages