January 28, 2014

UVCCM YAUNGA MKONO KAZI ZA SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
DAR ES SALAAM, Tanzania

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imeunga mkono kazi zinazofanywa na sekretarieti ya chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu Abdulrahaman Kinana huku ikiwatupia lawama baadhi ya vigogo kutokana na kukwamisha juhudi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda amesema, vijana wa UVCCM wanatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga chama kwa kusimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake.

Makunda alisema, inapofika wakati wasimamizi wa chama wanapoanza kupigwa  vita juu ya kusimamia kanuni za chama hii siyo sahihi.

“Haiwezekani matajiri na watu wenye uchu wa madaraka watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema kutakilinda chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu”Alisema.

Hata hivyo Makunda alisema, wanaobezwa leo  kuwa wanaharibu chama ndiyo wameweza kurudisha imani ya wananchi kwa chama , imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wa nchi hii.

Aidha Makunda alisema, mtu anayebeza ziara zilizofanyika na kuwaita viongozi walizozifanya ziara hizo ni waropokaji na wahuni anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.


“Muhuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo, hana maadili, asiyependa chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine” Alisema Makonda.
 Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
  Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko la Jumuiya ya Vijana wa CCM kuunga mkono kazi ya sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu, Mh. Abdulrahaman Kinana. 

No comments:

Post a Comment

Pages