January 03, 2014

WAAMUZI 11 WAPATA BEJI ZA FIFA
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewapatia beji waamuzi kumi wa Tanzania kwa mwaka 2014.

Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.

Waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.

WATATU WAOMBEWA ITC SHELISHELI
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.

Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.

TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment

Pages