February 01, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI MBEYA1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu. (Picha na Fullshangwe-Mbeya)1AKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya. 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Blogger wa Mbeya yetu Blog Bwana Joseph Mwaisango.

3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika meza kuu kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
4Waendesha Bodabona wakimshagilia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiongea nao leo. 5Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukitoka uwanja wa ndege wa Songwe kuelekea mjini Mbeya leo mara baada ya kuwasili mkoani humo. 6Shangwe za waendesha bodaboda zikiendelea. 7Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. 8Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. 9Waendesha Bodaboda wakifuatilia hotuba za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo. 10Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza wakati wa mkutano huo leo. 11Hapa ni Shangwe tu 12Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea risala ya waendesha Bodaboda kutoka kwa Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda.
13Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibebwa juujuu na waendesha bodaboda mara baada ya kuwahutubia kwenye ukumbi wa Mkenda leo. 14 





Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na uongozi wa waendesha Bodaboda kushoto ni mwenyekiti Vicent Mwashoma na kulia ni Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda

No comments:

Post a Comment

Pages