February 10, 2014

MAGARI ZAIDI YA 3000 YAKWAMA ENEO LA HEDARU BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA NA KUFUNGA BARABARA
 Baadhi ya wasafiri waliokwama wakiangalia greda inayojaribu kutengeneza njia ili waweze kupita. (Picha/Habari kwa hisani DJ Sek Blog) 
 Wasafiri wakiwa wamekwama eneo la Hedaru.
 Maroli na mabasi yakiwa kwenye foleni baada ya njia kuzibwa na mafuriko ya maji.
 Wakandarasi wakijadiliana jambo ili kuweza kupata ufumbuzi.
 Umati wa wasafiri wakiwa wanashangaa jinsi barabara ilivyozuiwa na maji.
Hii ndio hali halisi inavyoonekana malori yakiwa yamekwama katikati ya barabara.

Magari zaidi ya 3000 yamekwama mda huu eneo la hedaru baada ya barabara kufungwa na kuzibwa na maji mengi yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha eneo hilo.Wasafiri wamekwama eneo hili kwani magari na mabasi pia magari ya mizigo yanashindwa kupita kwa kuwa njia haionekani.



Kampuni ya ujenzi inayojenga barabara hiyo wanajitaidi kuchimba maeneo ya pembeni ili kuweza kuhamisha maji ili angalau njia iweze kuonekana.Hali ni mbaya eneo hili hivyo serikali inatakiwa kuwahi kwenda kutoa msaada wa kuweza kupunguza maji na hatimaye magari yaweze kupita.

No comments:

Post a Comment

Pages