February 16, 2014

Mchezo wa Mbeya City dhidi ya Simba wavunja rekodi ya Yanga Sokoine waingiza mil 105
KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya Mbeya City Juma Mwambusi amesema kuwa matokea ya sare ya 1-1,mchezo wa juzi dhidi ya timu yake na Simba ni moja chachu kwa kwa kujipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Coast Union mchezo wa utapigwa katika dimba la Mkwawani jiji Tanga.

Akizungumza na Tanzania Daima kocha  huyo amewatoa hofu wadua na masabiki wa wa timu kuwa ana imani mchezo utakao fuata timu hiyo itafanya vyema ili kujihakikishia mazingira mazuri ushindi na hatimaye kubeba ubingwa.

Mbeya City ilishika dimbani mwishoni mwa wiki dhidi ya Simba ,mchezo ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare kwa kufungana kwa bao 1-1 mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkali kutokana na Simba kupoteza mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Mgambo Shoting ya jiji Tanga.

Katika mchezo huo alioshudiwa na melfu ya mashabiki jumla shilingi mil 105,000,000/ zilizo uzwa kutokana na tikeki 21000 ambapo kila timu imeondoka na kitita cha sh 25,316,630.58.

Kwa mujibu wa msimamizi wa kituo Lwitiko Mwamundela alisema kuwa mbali kila timu kilamba kitita hicho mapato hayo yamevunja rekodi ya mchezo wa mazunguko wa kwanza kati ya Mbeya City na Yanga  ambao jumla ya sh mil 100 zilitakaikina kutoka na mauzo ya tiketi 20,000.

Aidha katika hatua nyingine Mwamundela alisema kuwa katika mgawanyo huyo VAT 16,016,949.15,gharama za uwanja 12,872,702.57,gharama za mchezo mil 7,723,621.52,Kamati ya ligi 7,723,621.52 sawa na asilimia 9.

Katika hatua nyingine Lwitiko aliongeza kuwa kwa upande wa TFF mgao wake ni sh mil 3,861,810.75 na chama cha Soka Mkoa ni sh 3,0003,630.58.

Hata hivyo licha ya mchezo huo kuingizi kiasi hicho ch afedha changamoto ni TFF ni na uchache wa tiketi ambao ulipekea mamia ya mashabiki kukaa nje ya uwanja na wengine kuparamia miti na waengine kukaa kwenye najengo marefu yalikaribu na uwanja huo kwa lengo la kushuhudia mchezo hadi muda ulipofika wa fungilia mbwa ndipo walipo ingia.

No comments:

Post a Comment

Pages