HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 14, 2014

NSSF YADHAMINI SEMINA KUHUSU JAMII KUPENDA KUFANYA MAZOEZI
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Maadili na Kazi limetaka jamii kujimudu kimawazo na kupenda kufanya mazoezi, kuepuka msongo wa mawazo.

Mwanzilishi wa Shirika hilo, Scholastica Kimaryo alisema hayo wakati wa semina iliyowakutanisha wadau mbalimbali.

Mada Kuu ilikuwa 'Kuunda maadili kuwa kiongozi bora kwa kujijua mwenyewe kiakili, kiroho na kimwili'.

'Alisema msongo wa mawazo mi tatizo kubwa kuliko Ukimwi'.

Dk. Kimaryo alisema kupitia ufadhili wa mashirika mbalimbali, ikiwemo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wamekuwa wakifundisha wafanyakazi jinsi ya kujimudu mawazo na kufanya mazoezi ili kupunguza tatizo hilo.

Aidha, alisema wamekuwa wakihamasisha jamii umuhimu wa  kuondokana na tatizo la msongo wa mawazo na kupitia elimu hiyo wengi wameweza kujitibu tatizo hilo.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Jumanne Mbepo akizungumza, wakati wa semina fupi kuhusu jamii kupenda kufanya mazoezi ili kuepuka msongo wa mawazo iliyoandaliwa na Taasisi ya Maadili na kudhaminiwa na NSSF.
Mabalozi na watu mashuhuli wakiwa katika semina hiyo.
Dk. Scholastica Kimaryo akitoa mada katika semina hiyo.



 Ofisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Devota  Ikandilo (kulia), akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake, wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na Taasisi ya Maadili inayosimamiwa na Dk. Scholastica Kimaryo ambaye akitoa mada juu ya kuunda maadili ambayo yatamsaidia mtu binafsi kuwa kiongozi bora jijini Dar es Salaam jana na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

No comments:

Post a Comment

Pages