February 19, 2014

Profesa Elisante: Milango iko wazi kwa Viongozi wa Vyama vya Michezo
 Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, Katbu Mkuu wa Chama cha Mchezo Tennis Tanzania (TTA), William Kallaghe na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao chao jijini Dar es Salaam.

Na  Frank Shija - WHVUM

Viongozi wa vyama vya michezo nchini wametakiwa kutmia fursa zilizopo kukutana na  viongozi wa Serikali ili kujadili kwa pamoja namna ya kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokutana Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe alipomtembele ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.

Profesa Elisante alisema kuwa ni vyema viongozi wa vyama vya michezo kushirikiana na Serikali katika kutafuta namna ya kuendeleza michezo nchini badala ya kukaa na kulalamikia pembeni.

Aidha amesema kuwa milango iko wazi kwa viongozi wa vyama vuya michezo kufika katika ofisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kuongeza kuwa atafarijika sana akiona kasi ya viongozi hao kutembelea Wizarani hapo ikiongezeka.

"Natao wito kwa viongozi wa vyama vya michezo nchini wajenge utamaduni wa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara hii ili kutafuta namna na njia bora ya kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini badala ya kukaa pembeni na kuiilaumu Serikali, kwakweli hii si sawasawa" Alisema Profesa Elisante.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ushirikiano ambao wamekuwa wanautoa kwa vyama vya michezo hapa nchini na kusema kuwa hii inaleta faraja kuwafanya kutokuwa wapweke.

Kallaghe aliongeza kuwa ni vyema sasa viongozi wa vyama vya michezo wakatambua umuhimu wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao mbalimbali.
Aliongeza kuwa atahakikisha anahamasisha viongozi wenzake kutumia fursa za kukutana na viongozi wa Serikali ili kukaa meza moja na kujadiliana namna ya kuboresha sekta ya michezo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages