February 07, 2014

SIKU 100 ZA TFF, MALINZI AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, kuhusu siku 100  tangu walipoingia madarakani. Kushoto ni Msaidi wa Rais wa TFF, Ufundi, Pelegrinius Rutahyuga na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura. 
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Mwandishi wa ITV, Hemed Kivuyo akiuliza swali wakati wa mkutano huo.

DAR ES SALAAM, Tanzania
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameelezea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Ilani yake siku 100 tangu alipoingia madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Februari 7 mwaka huu) katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi aliainisha maeneo kadhaa yaliyopewa kipaumbele na tayari yameanza kufanyiwa kazi pamoja na changamoto zilizopo.

Alisema muundo wa Idara ya Ufundi umebadilishwa kwa kuundwa vitengo vya ufundi, elimu na maendeleo ya mpira wa miguu huku maeneo ambayo tayari yameanza kufanyiwa kazi kuwa ni;

Ujenzi wa kituo cha mpira wa miguu (football centre of excellency), timu kupanda daraja, kuanzisha mashindano mapya na kufufua ya zamani, mpira wa miguu wa wanawake, maandalizi ya vijana (grassroot football), tiba, walimu na makocha, utawala, uhusiano na Zanzibar, klabu za mpira wa miguu, wachezaji, masoko na uwekezaji, kitengo cha habari, viwanja na timu ya Taifa (Taifa Stars).

Rais Malinzi amesema changamoto zilizopo kwa sasa ni matumizi ya tiketi za elektroniki, ufinyu wa bajeti, madeni, nidhamu, maadili na uchezeshaji wa waamuzi.

Ametoa mwito kwa wadau wote nchini wakiongozwa na Serikali, Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Afrika (CAF), Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), vyombo vya habari, mashirika ya umma na kampuni binafsi kushikamana na kuwa kitu kimoja kwa nia ya kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages