February 23, 2014

SIMBA YACHAPWA 3-2 NA JKT RUVU
 Golikipa wa JKT Ruvu, Shaban Dihile akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. JKT Ruvu ilishinda 3-2.
 Beki wa Simba, Issa Rashid (kulia), akichuana na mchezaji wa JKT Ruvu, Amos Mgisa  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.  JKT Ruvu ilishinda 3-2.
Kocha wa JTK Ruvu, Fred Felix ‘Minziro’ akitoka uwanjani ya pambano la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kumalizika, ambapo timu yake iliifunga Simba 3-2. 
 Kocha wa JKT Ruvu, Fred Felix ‘Minziro’ akiwa  amebebwa juu baada ya timu yake kuifunga Simba mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe (kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka beki wa JKT Ruvu, Nashon Naftali katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. JKT Ruvu imeshinda 3-2. 
Wachezaji wa timu ya JKT Ruvu, wakishangilia bao la pili la timu yao dhidi ya Simba wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. JKT Ruvu imeshinda 3-2.
Mashabiki wa Simba wakishuhudia timu yao ikipata kipigo.

No comments:

Post a Comment

Pages