October 22, 2014

KAMATI YA BUNGE HUDUMA ZA JAMII WAKAGUA MIRADI YA ILIYOFADHILIWA NA TEA KATIKA CHUO KIKUU CHA ARDHI DAR

 Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Kondoa Kaskazini Zabein Mhita akiongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii walipowasili katika Ofisi za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Baadhi ya wabunge wakiwa katika Ofisi za TEA kabla ya kunza ziara ya kukaguzi mradi wa ujenzi wa kumbi za mihadhara katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akizungumza na wabunge wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Kondoa Kaskazini Zabein Mhita akizungumza wakati walipofika katika Ofisi za TEA.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka akiwaonyesha wabunge wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii Ofisi za TEA zilizopo Mikochezi jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja.
Naibu Makamu Mkuu  Chuo Kikuu cha Ardhi, Taaluma, Prof. Gabriel Kassenga (kulia) akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge Huduma za Jamii walipofanya ziara ya kukaguzi mradi wa ujenzi wa kumbi za mihadhara jijini Dar es Salaam jana, ambapo Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetoa mkopo wa sh. milioni 600 katika kufanikisha ujenzi wa kumbi hizo. Kushoto ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Kondoa Kaskazini ni Zabein Mhita na wa tatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama. 
Jengo lililokamilika linavyoonekana kwa nje.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama (kushoto) akiangalia viti katika jengo lililokamilika.

No comments:

Post a Comment

Pages