October 17, 2014

KANISA LA CHRIST EMBASSY LATOA MSAADA WA KOMPYUTA KWA JESHI LA POLISI

Mchungaji wa Kanisa la Christ Embassy, Ken Igini akimuonyesha sehemu ya msaada wa Kompyuta 10 Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Siro baada ya kukabidhi kompyuta hixo. Kushoto ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Majambu. (Picha na Francis Dande) 
Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Siro, akimshukuru Mchungaji wa Kanisa la Christ Embassy, Ken Igini baada ya kupokea msaada wa Kompyuta 10 pamoja na vitabu mbalimbali vya dini ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Hafla hiyo ilifanyika Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Majambu. 
 Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Siro, akipokea sehemu ya msaada wa Kompyuta 10 kwa ajili ya vituo vitano vya Polisi kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa la Christ Embassy, Ken Igini (wa pili kushoto) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi  Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Majambu.
Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Siro, akipokea sehemu ya msaada wa vitabu vya dini kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa la Christ Embassy, Ken Igini. kulia ni Balozi  Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Majambu.
 Balozi wa Nigeria, Dk. Ishaya Majambu (wa pili kulia) akiwa na mkewe wakiimba nyimbo za kumsifu mungu. Wa tatu kulia ni Mchungaji wa Kanisa la Christ Embassy, Ken Igini na Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Siro.
Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Siro akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo.

Na Mwandishi Wetu


Jeshi la Polisi jana lilipokea msaada wa Komputa 10, biblia 500 pamoja na vitabu mbalimbali vya dini kutoka Kanisa la ‘Christ Embassy Tanzania’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea msaada huo, Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, alisema anashukuru sana kwa msaada huo ambao utasaidia kutatua baadhi ya changamoto walizokuwa nazo pamoja kulinda watu na mali.

Alisema bado changamoto ni nyingi katika Jeshi hilo, vitendea kazi havijitoshelezi, hivyo amewaomba wadau wajitokeze kutoa misaada.

“Misaada inasaidia sana, kupitia msaada huu tutaweza kutunza kumbukumbu za wahalifu kwa urahisi zaidi, lakini bado hautoshi kwani changamoto ni nyingi hivyo tunaomba wadau wajitokeze kutusaidia ili kuboresha ufanisi katika kazi,” alisema.

Aidha Sirro ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu au mhalifu. 

“Wananchi watoe taarifa za uhalifu au mtu yeyote ambaye ni mhalifu, wao ndio wanaowajua na wanaishi nao katika mazingira yanayowazunguuka,” alisema.

Naye Mchungaji wa Kanisa hilo kutoka Nigeria ambao wako nchini kwa ajili ya kusambaza dini, Ken Igini alisema lengo la msaada huo ni kuadhimisha siku ya Mwalimu Nyerere, na msaada huo si kwa Jeshi la Polisi tu bali kwa nchi nzima.

“Leo tumeanza na Polisi, kesho tutaenda kutoa biblia 1000, nguo pamoja na sabuni kwa wafungwa. Tunaamini neno la Mungu litasaidia kubadilisha watu hawa hata watokapo gerezani na nguo zitawasaidia pia wakitoka humo,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages