October 14, 2014

‘Kasisi ampiga Stop Makamba asihubiri msibani’

Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Alhaji Yusuf Makamba akiwa kwenye Msiba wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Ernest Masima kijijini kwake Chibelela.


Na Bryceson Mathias, Chibelela Bahi

KASISI Ujumla (Vicar General), George Chomola, wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dodoma, Jumapili Oktoba 12,  katika Kijiji cha Chibelela, alimpiga ‘Stop’ Katibu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Alhaji Yusuf Makamba, asihubiri kwenye Msiba wa,  Ernest Masima,.

Akizungumza kabla ya kutoa Mahubiri ya Neno la Mungu alilolisoma, Chomola ambaye ni Kasisi wa Ujumla wa Makasisi wa Kanisa hilo mkoani Dodoma alisema, “Nimemuona Alhaji Makamba, tafadhali tumia dakika Moja utoe Salamu za Rambirambi kwa Waombolezaji, ‘ila Usihubiri’.

Pamoja na kupigwa ‘Stop’ Makamba hakukidhi Marufuku hiyo ya kutumia dakika moja na badala yake alitumia dakika tatu, akielezea Jinsi ambavyo walifanya kazi na Marehemu ambaye hadi kifo chake alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Samwel John Malecela, ambaye alituma salamu za Sauti toka nje ya aliko, walieleza jinsi ambavyo CCM kimempoteza mtu kiliyemtegemea katika kuimarisha Chama na Ushauri,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima, amabaye ni mdogo wake na Marehemu alisema, “Ukiona Paka anamkejeli Paka ujue yuko karibu na Shimo; Familia kwa Muda mrefu tulijivua Kaka yetu, ambaye muda mwingi aliutumia kwenye siasa, ingawa mimi siwezi na simfikii.

“CCM kimempoteza Mtu makini, Jamii imempoteza Mshauri, Kanisa limempoteza Mtendaji, na sisi Familia tumempoteza Jembe, kwa sababu alikuwa akila Pilipili (Mambo Magumu) kama anakula asali (akiyafanya mepesi,

Aidha Mdogo mwingine wa Marehemu, Mchungaji, Noah Masima, aliuomba radhi umati wa waombolezaji uliohudhuria mazishi hao akisema, “Mtusamehe, sisi familia, tulikuwa tukishindana wenye kwa wenyewe kuhusu kukosekana kwa marehemu nyumbani, kumbe alikuwa akiwatumia ‘tumewaona’.

No comments:

Post a Comment

Pages