October 11, 2014

Mapendekezo yawasilishwa kwa uongozi wa Benki ya Dunia

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo.
 Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kuhusu hali halisi ya misaada.
 Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kuhusu hali halisi ya misaada.
 Ujumbe kutoka Tanzania ukimsikiliza kwa makini  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose Mkurugenzi Mtendaji mpya anayeachiwa kiti.
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakiwaangalia kwa mshangao wakurugenzi hao wawili walipokuwa wakiingia hawapo kwenye picha.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Katika mkutano muhimu uliofanyika jioni hii hapa mjini Washington DC. Kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika pamoja na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo ulimpatia nafasi nzuri sana Dr. Likwelile kuweza kueleza mambo muhimu ambayo Benki ya Dunia ingepaswa kuyafahamu.

Katika mawasilisho yake katibu Mkuu huyo aliwaeleza viongozi wa Benki ya Dunia kuwa ,anashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao ameupata kutoka Benki ya Dunia na kusema kuwa hii imeisaidia sana Tanzania katika kupiga hatua kiuchumi. Akiendelea kuzungumza Dr. Likwelile alisema kuwa pamoja na kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na tatizo ambalo lina sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti.

 Hili amelieleza kuwa linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo yanayohusu IPTL kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye makubaliano. “ IPTL haina uhusiano na makubaliano ya awali suala hili limeingia katikati hii inaathiri utekelezaji wa kibajeti.”alisema.

 Aidha aliendela kueleza kuwa sera ya Benki ya Dunia inadai kuwa kabila la Kimasai limetengwa na hivyo kutaka baadhi ya miradi isiende sehemu nyingine zaidi ya umasaini, hii nayo ni changamoto nyingine”. Katika mazungumzo hayo ilionekana kweli kuwa kwa kuchelewesha kutoa fedha kwa ajili ya miradi kunachangia sana kurudisha nyuma maendeleo.

Kwa mapendekezo haya mawili makubwa kama yatafikishwa kwenye ngazi ya juu na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu itapiga hatua kama ilivyojipangia. Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo kwa mikono miwili na wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi.

Hali ya hewa mjini hapa ni ya baridi na manyunyu ya hapa na pale.

Imetolewa na: Ingiahedi Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha Washington D.C 10/10/2014

No comments:

Post a Comment

Pages