Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) ambaye pia ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitoka katika Chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kulekea katika Gereza la Segerea baada ya kukosa dhama katika kesi inayoamkabili pamoja na wanachama wenzake ya kutotii
amri halali ya Jeshi la Polisi na kufanya mkusanyiko usio halali.
Halima Mdee akielekea kupanda gari la Polisi kuelekea Gereza la Segerea huku akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima
Mdee akipanda gari la Polisi kuelekea Gereza la Segerea, baada kukosa dhamana
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Halima akipanda gari la Polisi tayari kwa safari ya kuelekea gereza la Segerea.
Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya Mahaka ya Hakimu Mkhazi Kisutu wakati wa kesi ya Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) ikisikilizwa mahakamani hapo.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee (katikati) akiwa na watuhumiwa wenzake muda mfupi kabla ya kuelekea Gereza la segerea.
FFU wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya Kisutu.
Askari wa FFU akiwa nje ya Mahakama kuhakikisha usalama unakuweo wakati wa kesi ya mbunge wa Kawe ikiendelea.
Safari ya Segerea inaanza.
Magari yakitoka Mahakamani.
Baadhi ya wanachama na wafuasi wa Chadema waliofika Mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo wakipaza sauti zao.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MBUNGE wa
jimbo la Kawe, Halima Mdee (35), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
pamoja na wenzake nane, wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutotii
amri halali ya Jeshi la Polisi na kufanya mkusanyiko usio halali.
Mdee ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema (Bawacha), alifikishwa
mahakamani hapo na wenzake na kusomewa mashitaka na jopo la Mawakili
watatu wa Serikali wakiongozwa na Bernad Kongola, Salum Mohamed na Hellen Mushi,
mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda.
Mawakili hao
waliwataja washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Rose Moshi (45) mkazi
wa Kinondoni (b), Renina Peter maarufu kama (Lufyagila) mkazi wa kinondoni
mkwajuni.
Wengine ni Anna
Linjewile (48), mkazi wa Mbezi Luis, Mwanne Kassim (32), mkazi wa Pugu Kajiungeni,
Sophia Fanuel (28) mkazi wa Mbezi Beach, Edward Julius (25) mkazi wa Msasani, Martha
Mtiko(27) mkazi wa Mikocheni na Beauty Mmari (35) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni.
Akiwasomea
shitaka la kwanza, Wakili Kongola alidai kuwa Mdee na washitakiwa wenzake,
mnamo Oktoba 4, 2014, mtaa wa Ufipa, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, bila ya kuwa na uhalali
walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mratibu wa Polisi(SP),
Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi hilo.
Kongola
alidai kuwa washitakiwa hao, walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 124 cha
sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Wakisomewa
shitaka la pili na wakili Mohamed, siku hiyo ya tukio katika eneo hilo,
washitakiwa hao kwa pamoja, walifanya mkusanyiko usio wa halali kwa lengo moja
la kwenda kwenye Ofis ya Rais.
Wakili huyo
alidai kuwa, kosa hilo ni kinyume na Kifungu cha 74 na 75 cha Sheria ya Kanuni
na Adhabu, sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Washitakiwa
hao walikana mashitaka hayo, upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi
umekamilika, hivyo waliiomba mahakama kupanga tarehe ya kuwasomea washitakiwa
maelezo ya awali (PH).
Kaluyenda
alidai , dhamana ya washitakiwa hao ipo wazi ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye
barua za ofisi wanazofanyia kazi pamoja na kitambulisho , huku wakitakiwa kutoa
bondi ya sh. milioni moja kwa kila mshitakiwa.
Washitakiwa
hao walirejeshwa rumande baada ya wakili kushindwa kumaliza kuhakiki fomu za
dhamana zao.
Aidha, washitakiwa
hao waliondolewa kwenye ardhi ya Mahakama ya Kisutu wakiwa chini ya ulinzi
mkali wa zaidi ya polisi 30 na msafara wa magari manne likiwemo la maji ya
kuwasha.
No comments:
Post a Comment