October 18, 2014

MTUMISHI WA HALMASHAURI AKUTWA AMEKUFA CHUMABANI KWAKE

Na Ibrahim Yassin, Rungwe

MTUMISHI wa Halmashauri Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilayani Rungwe mkoani Mbeya Benjamini Kaswaga (50) amekutwa amekufa chumbanii kwake tarehe 16/10/2014 aligundulika na majirani majira ya saa mbili usiku baada ya kuona hakutoka nje ya nyumba yake tangu alipoingia.

Akizungumzia tukio hilo kwenye kikao cha Baraza la madiwani kilicho keti jana mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Vironica Kessy alisema katika uhai wake Benjamini alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka na kwamba kifo chake uenda kimetokana na tatizo hilo.

Alisema kuwa mtumishi huyo hakuwa na mke hivyo kutoonekana kwa siku mbili huku mlango wa nyumba yake ukiwa umefungwa ndipo majirani walianza kuwa na shaka ambapo walipo sogea walisikia harufu mbaya ikitoka katika nyumba hoyo na kuamua kutoa taarifa polisi.

Aliongeza kuwa jeshi polisi wilayani humo lilifika eneo la tukio na kuamuru kuvunja mlango mbele ya wananchin wakiwa na viongozi wa kijiji ambapo wakuta mtumishi huyo amekufa na kwamba baadaye mwili huo ulipelekwa hadi kwenye hospital ya wilaya kwa uchunguzi.
 
Mganga mkuu wa wilaya Ndagabwene Sungwa alisema tatizo la kifo cha mtumishi huyo hawezi kulitolea maelezo.

Madiwani na watendaji katika halmashauri hiyo wameambatana na familia hiyo kwenda katika maandalizi ya mazishi ya mtumishi huyo yatakayofanyika kesho wilayani humo na kusema kuwa walimpenda lakini mungu alimpenda zaidi,

No comments:

Post a Comment

Pages