October 18, 2014

Mwenyekiti amkaribisha DC Chadema

Na Bryceson Mathias, Chalinze

MWENYEKITI wa  CHADEMA Korogwe, Mjumbe wa Baraza Kuu na na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Aulelian Nziku, amempongeza na kumkaribisha Chadema Mkuu wa Wilaya, Mrisho Gambo, ashiriki kukomesha Rushwa na Ufisadi nchini, huku akidai amekumbuka Shuka Asubuhi.

Akizungumza wakati anarudi toka kwenye kikao cha watia nia ya Ubunge Chadema Dar es salaam, Nziku alisema anampongeza Gambo kwa sababu amefanyia kazi Kelele za Chadema Majukwani, ambapo kelele hizo zilimfikisha Tume ya Maadili ya Umma kuhojiwa.

Nziku alisema, Sababu za Gambo kupongezwa na Chadema Korogwe zinatokana na hivi karibuni kutakiwa kukamatwa afikishwe kwenye Baraza hilo kwa kile kinachodaiwa na wananchi aliwatia Lupango Wenyeviti na Watendaji waliotafuna fedha za Ujenzi wa Maabara.

Aliongeza kuwa, “CCM Gambo hakumfai, na aelewe Sababu za Wananchi Korogwe kumpokea kwa Nderemo akitoka Baraza la Maadili walikomtosa wana CCM wenzake, kunatokana na kufanyia kazi Kauli za Chadema Majukwani, kuhusu umizigo wa watendaji na wenyeviti hao.

“Chadema tuliahidi na tutafanya; Kutawataja hadharni Watendaji, Wenyeviti, Madiwani, Wabunge, na Wakurugenzi Mizigo katika Wilaya yetu, wanaokwamisha Maendeleo ya Wilaya kwa Dhuluma, Rushwa, Ufisadi na kutafuna fedha ya ‘Umma Hovyo hovyo’”.alisema Nzilu

Alisema, ukiona Panya anamtunishia Paka Misuli, Ujue Shimo la kukimbilia lipo karibu; hivyo wana CCM kama Gambo, wanaofanya kazi ya kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa haki zao na Wenyeviti na Watendaji, wasiogope wanapotishwa; Wabwatuke, Kimbilio lao ni Chadema tuunganishe Nguvu’.

Aidha alisema, anategemea kuwaanika Viongozi, Mgambo, Wenyeviti na Watendaji wa Kijiji cha Kwamkole, Kata ya Kizara, Tarafa ya Magoma, waliomfunga Kamba Mwananchi kwenye Mti, eti sababu hakutoa fedha za Maabara, wakiwa na risiti Feki. “Huu si Unyama ule wa Ujangili”.alihoji Nziku.

No comments:

Post a Comment

Pages