October 06, 2014

TAHLISO WATAKA MIKOPO KWA WOTE

JUMUIYA ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini (Tahliso), imeshangazwa na kauli ya Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Profesa Sylivia Temu, kwamba wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haiwezi kutekeleza madai ya wanafunzi hao hadi itakapopata barua rasmi.

Kauli ya Profesa huyo inakuja siku chache baada ya taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Tahliso kupitia vyombo vya habari kuhusu maombi yao ya kuongezewa fedha za kujikimu kutoka sh 7,500 hadi sh 15,000 kwa siku kutokana na madai ya kupanda kwa gharama za maisha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa Tahliso, Mussa Mdede, alisema anamini wizara inazo taarifa rasmi ikiwemo ile ya kuwapatia wanafunzi wote 58037 waliomba mkopo.

Alisema kauli ya Profesa huyo haina ukweli kutokana na jumuiya hiyo ikiwa katika mkutano mkuu mkoani Iringa, Setemba 26 mwaka huu, ilituma Fax ya maazimio ya mkutano huo kwa waziri wa wizara hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Aliyataja baadhi ya maazimio hayo kuwa ni masuala ya vyuo kuwapandishia wanafunzi ada kiholela vikikiuka maagizo ya TCU.
“Tunapinga kauli ya Bodi ya Mikopo kutoa mkopo kwa wanafunzi 30,000 huku wengine 28,037 wakikosa, sasa maazimio yetu tuliyoazimia tunataka wote wapate mikopo bila kubaguliwa.

“Kwa kuwa niko safarini mkoani Mwanza, nimemuagiza katibu mkuu wa Tahliso kuwa anahakikishe kabla jua halijazama leo kwamba anaifikisha barua hiyo wizarani,”alisema kwa njia ya simu.

Mdede, alisema licha ya mambo yote hao, bado dhamira yao nikukutana na waziri wa wizara hiyo ili kuzungumzia mustakabali wa elimu ya juu nchini. 

No comments:

Post a Comment

Pages