October 20, 2014

WATANZANIA WAISAPOTI MASHADAVILLE MUSIC ENTERTAINMENT(M.M.E) NA SANAA NCHINI,KUNA STUDIO YA MUZIKI,GRAPHICS DESIGNING,KUDESIGN MAVAZI NA VIDEO PRODUCTION





KINGBIGY(Mkurugenzi wa M.M.E)

KAMPUNI chipukizi  inayojihusisha na uandaaji wa kazi za Sanaa ndani na nje ya nchi,Mashadaville Music Entertainment(M.M.E)  imewataka watanzania wafanye kazi na kampuni zenye uwezo na siyo kufuata majina.

Akizungumza na MUZIKI BEGANI ofisini kwake Ilala Jijini Dar es Salaa jana Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Moses Hayatta ‘Kingbigy’ alisema, watanzania wanapaswa kufanya kazi nzuri, zenye ubora Zaidi kuliko kufanya kazi zisizo na viwango na makampuni yenye majina makubwa.

“Watanzania wanapaswa kufungua macho na kuzisapoti kampuni changa za Sanaa kama Mashadaville Music Entertainment (M.M.E) ili kuifanya Sanaa yetu izidi kusonga mbele na siyo kufuata majina ya makampuni ambayo hudidimiza Sanaa nchini kwa kufanya kazi duni”.Kingbigy alisema

Vilevile Kingbigy aliongeza  kuwa kampuni hiyo inayofanya kazi za kurekodi muziki wa aina zote audio na video,kutengeneza matangazo aina yote ,Kubuni na kutengeneza mavazi ina matawi manne ambayo majina yake yapo kwenye mabano ni ya matangazo(Graphics Solution), kurekodia audio (Bass Station Record),kurekodia video(Black Diamond Videos) naya kubuni mavazi(Wavikaji Clothing Line) makao yake makuu yako ilala msaada gereji Dar es Salaam.

Kingbigy alisisitiza kuwa katika uandaaji wa muziki na video za muziki,tayari wameshanya kazi na wasanii kibao wakubwa  wakiwemo Chibwa, Spince Seseme, Sumaryder, Vedasto, Yuzzo, K.C.K na Kelvo 101.


Vile vile katika upande wa matangazo Kingbigy alisema, wameshafanya kazi na makampuni kama Real Insurance, Keviant, Vigor, E fm, Buja eyes, Rema Tv, Salama Tv na Primus Beer.
0715-577805

No comments:

Post a Comment

Pages