October 30, 2014

WAZIRI WA FEDHA -SAADA MKUYA AZINDUZI WA CHAPISHO KUU LA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI 2011-2012-TANZANIA BARA


Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (Katikati) akionyesha kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Ofisa kutoka Shirika la Maendeleo la DPG, Sinikka Antila, Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.  Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Veronika Kazimoto (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (katikati).

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa akimfafanulia jambo Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum mara baada ya kufanya uzinduzi.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akimkabidhi chapisho Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.

Wawakilishi toka Mashirika mbali mbali ya Kimataifa wakiwa katika picha ya pamoja.
Meza kuu ikifuatilia kwa makini.
Wanafunzi wa Chuo cha Takwimu nao walifika.
Wawakilishi toka mashirika ya kimataifa nao walifika.
Picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages